METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, December 2, 2021

SAFARI YA NDOTO YA NYERERE KUWAUNGANISHA WATANZANIA

Mzee Frances Khatibu ambaye alishiriki katika harakati za Uhuru wa Tanzania, katika uzalishaji na uanzishwaji wa Kijiji cha Ujamaa cha Kerege Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani mwaka 1964, Mzee Khalid alitolewa Nanchingwea Mkaoni Lindi.

Bi. Kashinde Mohamed Kigwande ambaye Mume wake alitolewa Nanchingwea Mkaoni Lindi,  alishiriki katika harakati za Uhuru wa katika uzalishaji na uanzishwaji wa Kijiji cha Ujamaa cha  Kerege Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani mwaka 1964.

Mzee Jumaa Ismail ambaye alishiriki katika harakati za Uhuru wa Tanzania, katika uzalishaji na uanzishwaji wa Kijiji cha Ujamaa cha Kerege Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani mwaka 1964, Mzee Isamail  alitolewa Masasi  Mkaoni Mtwara.

PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO

Na Judith Mhina- Maelezo 

Maneno hayo yalitamkwa na Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika na Rais wa Jamhuri ya Tanganyika na baadaye  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwa ni siku  adhimu na muhimu kwa Watanganyika katika maisha yao yote kukumbuka Tarehe 09 Desemba, mwaka 1961, sherehe zilizofanyika pale  uwanja wa Taifa sasa Uhuru Jijini Dar-es-salaam.

Naam, sherehe za Uhuru wa Tanganyika kuanzia hapo zimekuwa zikiadhimishwa mwaka hadi mwaka kukiwa na kauli mbiu mbalimbali kulingana na wakati na majukumu yanayoikabili Taifa kwa kipindi hicho kama mwaka 1961 kauli mbiu ilikuwa “Uhuru na Kazi”.

Uhuru na Kazi inatukumbusha  moja ya maandiko ya Mwalimu Nyerere ametambua  na kuona zipo  dalili za kupuuzwa  kwa baadhi  ya fikra  na mawazo yake muhimu na msingi imara kwa  Watanzania  kamwe hawatakiwi kuzipuuza  Mwalimu alisema 

“Wapo watu wengi wema wanaoamini kuwa hizo fikra ambazo katika nchi hii zinahusishwa na jina langu sasa zimekufa na ni sawa zizikwe. Hamuwezi kushangaa kusikia kuwa sikubaliani nao!. Fikra nzito hazifi kwa urahisi hivyo: zinabaki zikikera, na kila jamii ya binadamu katika historia inajipalia makaa kwa kuzipuuza”.  (J.K. Nyerere) 

Fikra hizo muhimu na za msingi  mojawapo ni  “Uhuru na Kazi” ambapo haikuwa  kazi ya Mwalimu Nyerere peke yake kuhimiza wananchi kufanya kazi  kwa bidii na kuacha kubweteka wakidhani sasa tupo huru kila jambo litafanyika  na kufanikiwa bila kutoa jasho na kujituma. Hivyo nguvu ya pamoja ya viongozi ndani ya Jamhuri ya Tanganyika na baadaye Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ilitumika kuwakumbusha na kuwaasa kutobweteka na kudhani Mwalimu ndio suluhisho la kila kitu bila kufanya kazi.

Katika suala hilo hilo la “Uhuru na Kazi” sherehe za Uhuru wa Tanganyika mwaka 1964 zilizofanyika Jijini Dar-es-salaam katika hotuba yake aliyoitoa kabla ya kumkaribisha Mwalimu Nyerere kuongea na wananchi Makamu wa Kwanza wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Shekhe Abeid Amani Karume  alisema 

“Kazi aliyochukua Mwalimu Julius Nyerere kwa muda wote matawi yake ndio haya mavuno yake ndio haya, sasa tufanye nini tunarejea kwa Mwalimu Nyerere oohhhh!!! Ofisi bwana Oohhh!!!  Imemhusu wapi haya hii kazi yetu wenyewe!!! Uhuru na Kazi uhuru umepatikana katika nchi, Uhuru ukishapatikana katika nchi si kazi ya mtafuta uhuru peke yake maana lile lililokuwa linatafutwa limeshapatikana sasa tugawane huyu apite huku, apite huku tunafanye nini?” 

“Tufanye kazi kwa bidii kupiga vita adui uvivu na uzembe,  sio kukaa migahawani unataka Mwalimu Julius Nyerere aondoe njaa yote Tanganyika kesho, aondoe umasikini wote kesho, aondoe kila shida kesho, maji ya chumvi yageuke baridi kesho!! Inawezekana? Eheee!!! Tazameni nyie wananchi itazameni hii Tanzania yenyewe ina koloni wapi? Ehh!! Alah!!! sasa wewe unakaa mgahawani basi unalaumu tu koloni yetu la Tanzania wapi? Ehe!!! Hata leo tumalize kila kitu kwa siku moja, nadhani makosa makosa. Tushirikiane sote kufanya kazi kwa bidii mafanikio lazima yatafikiwa Eheeeeeeee!!”.  

Hayati Makamu wa Rais aliongeza na kusema “Eheee tunataka kufahamu nini maneno ya mikahawani hayaleti maana duniani leo Tanzania yetu tufanye kazi yetu kwa bidii. Tufanye kazi yetu kwa bidii, kwa sababu kila kitu tunacho wenyewe mikononi mwetu tutaweza kumaliza kila shida zetu kwa muda wetu utakaokuwa, madhari tunafanya kazi kwa bidii itakuwa.  Leo tumekuja kuzungumza na nyie ndugu zangu habari ya mikahawani tusisikie hayatiiwi maanani”.

Mwalimu Nyerere hakika tunakubaliana na wewe asilimia mia  kuwa fikra hizo nzito na mawazo yako  tangu tupate uhuru mwaka 1961 ni kweli ‘Uhuru  na Kazi’ Hivyo, kila Awamu ya uongozi iliyoingia madarakani tangu mwaka 1985 inaendelea  kusisitiza  kafanya kazi kwa bidii  na maarifa ili kuhakikisha nchi yetu ya Tanzania inapata mafanikio katika nyanja zote ili kuwe na ustawi wa jamii ya Kitanzania inayoheshimika duniani.

Kitabu cha Nyerere cha ‘Uhuru na Umoja’ ukurasa wa 309 amesema “Fikra makini pekee za matatizo yetu na matumizi ya fikra za kisayansi na malengo vinaweza kutuwezesha kufikia maisha bora tunayoyapigania”.

Hakika ni safari ndefu ya mafanikio ya nchi ya Tanzania kutoka 1961 hadi leo 2021 miaka 60 nchi inastahili kujipongeza kwa hatua tuliyofikia ya kuingia katika ‘Uchumi wa Kati’ mwaka 2020 miaka mitano kabla ya makisio ya wachumi wabobezi na matarajio ya wale wanauiangalia na kuifuatilia Tanzania popote walipo duniani.

Haya ni matokeo ya Uhuru na Kazi kamwe Watanzania tusibweteke na kuthani kuna Mjomba au Shangazi atakayekuja kufanya kazi na kutuletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja, familia na Taifa kwa ujumla  

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com