Na Nathaniel Limu – SINGIDA
Unaweza
ukawa unafahamu kuwa CHAMA cha mapinduzi (CCM) ni kama chama tawala nchini Tanzania Lakini
unapaswa kufahamu CCM ni chama cha pili ambacho kimekaa madarakani kwa muda
murefu baada ya chama cha TRUE WHIG PARTY TWP cha Liberia kwa
ukanda wa afrika kilichoanzishwa 1869 . CCM siyo tu chama tawala nchini Tanzania
bali ni cha ambacho kimedumu madarakani kwa miongo mingi na hakijapata misuko
suko ya kutishia uhai wake.
Chama
hiki kilichoasisiwa na hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kimezaliwa
mapema katika miaka ya 1977 ikiwa ni zao la muungano chama cha TANU ambacho
kilikuwa upande wa Tanganyika na AFRO- SHIRAZI PARTY ASP Kutoka visiwani Zanzibar
kisha kuungana na kuunda chama kimoja ambacho ni Chama Cha Mapinduzi CCM kinachotambuliwa
hadi sasa vizazi na vizazi ingawa mwaasisi alikuwa ni baba wa taifa Hayati
Mwalimu Julias Nyerere alieU ilikomboa
nchi kutoka mikononi mwa wakoloni
Waingereza.
CCM
katika chaguzi mbalimbali ikiwemo chaguzi kuu, kimekuwa kikigaragaza vyama vya
upinzani na Ushindi mnono wa CCM unatokana na kuwa na ilani thabiti ya uchaguzi,
inayo watetea maslahi ya wananchi
hususani wale wanyonge kupitia viongozi
wenye utu utakumba Mwenyekiti wa kwanza wa ccm Mwalimu nyerere ni moja ya
viongozi waliotengeneza msingi mizuri ya viongozi wa chama na serikali ambao
wamekuwa ni kichocheo cha utekelezaji wa ilani za chama hiki kikongwe.
Kupitia
ilani hiyo, CCM imekuwa ikishinda mapema asubuhi. Katika chaguzi zote, ushindi
wa CCM haujawahi kutiliwa mashaka. Hali hiyo imekuwa ikiwapa jeuri wenye chama
hicho, wanachama na mashabiki wake. Hili kundi limekuwa likiwatambia watani zao
(Upinzani) kwa wimbo unaomalizia kwamba ‘Wataisoma
namba’ pindi wanapopanda katika
majukwaa ya kisiasa , amewahi kusema alikuwa mwenezi wa ccm 2015-2020 ambeye
kwa sasa ni Mbunge Mteule Ndugu Humphey Polepole kuwa ccm wanachapa kazi wapinzani wamebaki na
kauli ya kuminywa kwa demokrasia lakini hawana hoja ya msingi ndio maana kwa
sasa wananshindwa kihalali na CCM.
Jeuri
nyingine ya CCM, ni ile ya kuunda serikali makini na inayowajali zaidi
wanyonge. Wana CCM na baadhi ya wasio wana CCM, wameendelea kukunwa na
utekelezaji wa ilani hizo. Pia wanakunwa na utumbuaji wa viongozi wasio
waadilifu au wanaojinufaisha kupitia mali ya umma.
Uchaguzi
mkuu uliopita wa 2020, CCM mkoa wa Singida ilikomba karibu nafasi zote za
udiwani,ubunge na Rais alipata kura za kutosha huku ikiwaacha wapinzani wake
wakigawana kura kiduchu mno.Jimbo la Singida mashariki lililokuwa mikononi mwa
CHADEMA,lilirejeshwa kwa kishido mikononi mwa CCM.
CCM
ya sasa ya awamu ya sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imejiongeza kwa
mambo mengi ya maendeleo.Hasa katika kuondoa kero na changamoto zinazowakabili
wananchi wanyonge.Kujiongeza huko,ni pamoja na
kuziagiza kamati za siasa ngazi ya mkoa, kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ya wananchi mara kwa
mara. Ukaguzi huo ujikite kubaini iwapo utekelezaji wa miradi hiyo, utafanana
na thamani ya fedha zilizotumika, na si vinginevyo.
kamati ya siasa mkoa wa Singida pamoja na kufanya vizuri kwenye kaguzi zake, na yenyewe imejiongeza. Imejiongeza kwa kuziagiza kamati za siasa wilaya, nazo ziwajibike katika kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ya wananchi. Endapo zitabaini ubadhilifu wo wote,wawajibishe wahusika.
Mwenyekiti
CCM mkoa Alhaji Juma Kilimba, amesema kaguzi za kamati za siasa wilaya, zina
faida nyingi. Amefafanua zaidi kwamba faida za kaguzi hizo za mkoa na wilaya,
ni pamoja na kuchukua hatua mapema kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.
Mapema
julai mwaka huu (2021) mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge, aliitisha
kikao maalumu kwenye ukumbi wa mikutano wa VETA mjini Singida.kutoa taarifa ya
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi CCM, katika kipindi cha Julai mwaka 2020 hadi
juni mwaka huu (2021). kikao hicho kimeweka rekodi ya kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa CCM na waalikwa mbali
mbali.
Katika
utangulizi wake mkuu huyo wa mkoa amesema ilani ya uchaguzi ya Chama Cha
Mapinduzi, ni tamko na ahadi maalumu zilizotolewa wakati wa kampeni za uchaguzi
mwaka 2020.
Amesema
CCM kilimteua/mchagua Hayati Dk. John Pombe Joseph Magufuli, kuwa mgombea
nafasi ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakati Rais wa sasa awamu
ya sita Samia Suluhu Hassan, alikuwa mgombea mwenza.
kupitia
Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, CCM ilitoa ahadi
za kuendelea kulinda uhuru, kuimarisha Muungano, kulinda Tunu. Tunu hizo za
kitaifa ni pamoja na falsafa ya mwenge wa uhuru. Vile vile kuendelea kujenga
taifa imara linalojitegemea kiuchumi na kisiasa
“amesema Dk. Mahenge.
Ameongeza
kwamba utekelezaji wa Ilani ya CCM ya uchaguzi wa dira ya taifa ya maendeleo
2025.
Aidha,
amesema unaenda sambamba na mpango wa maendeleo ya taifa (2021/2022-2025/2026.
Na mwongozo wa mfumo wa fursa na vikwazo kwa maendeleo (O and OD).Dk. Mahenge alisema
“Na vile vile Serikali imeendelea kuboresha
miundombinu, kupanga matumizi bora ya ardhi, utoaji huduma bora za kijamii
zinazojumuisha elimu,afya na maji. Kuimarishamakusanyo ya mapato ya ndani ya
mamlaka za Serikali za mitaa. Kama hiyo haitoshi, tumeimarisha masuala ya
utawala bora, kuboresha mazingira ya kufanyia kazi,” amefafanua zaidi Dk. Mahenge ambaye
ameahidi atahakikisha Mkoa wa Singida, unapaa kimaendeleo.
ILANI YA CHAMA KUHUSU
MAENDELEO KWA MKOA WA SINGIDA
‘HALIYA KIUCHUMI’
Ni
wazi ilani ya ccm inatekelezwa kitaifa itakubukwa katika kitabu cha ilani
katika uchaguzi wa mwaka 2020 kikiwa na kurasa zaidi ya 300 kilibainisha mambo
mbalimbali ya maendeleo , Dk. Binilith Mahenge Mkuu wa mkoa wa singida, alisema
asilimia 80 ya wananchi mkoani humo, wanajishughulisha na shughuli za kilimo,
ufugaji na uvuvi ambapo kwa sasa usalama ndani ya mkoa, umeimarika na kuwezesha
wananchi kutekeleza majukumu yao ya kiuchumi na kijamii kwa amani na utulivu
mkubwa.
“Hali hii imewezesha
hali ya uchumi kuwa na mafanikio mbalimbali. Mafanikio hayo ni pamoja na kukua
kwa pato la mkoa (GDP) kutoka shilingi trioni 2.6 kwa mwaka 2019 hadi kufikia
shilingi trioni 2.7 mwaka 2020. Na kukua kwa pato la wastani la kila mtu kwa
mkoa wa Singida kutoka shilingi 1.5 milioni mwaka 2019 hadi kufikia shilingi
1.6 milioni kwa mwaka 2020”. amesema.
Utekelezaji
wa ilani umeoneka kuwa chanya na inathibitishwa na Dk. Mahenge ambaye ametaja maboresho
ya matumizi ya ardhi vipande 10,481 kati ya lengo la vipande 3,500 ambayo ni
sawa na asilimia 299 ni miongoni mwa mambo yalitekelezwa kiuchumi kwenye ilani
hiyo.
‘MIUNDOMBINU’
Mtoto au Mjukuu wangu akiamka usingizini na kuniuliza kwa CCM imekaa Madarakani muda mrefu Nitamkumbusha tu msemo wa waswahili usemao ‘Wali wa kushiba utauona kwenye sahani ‘ CCM ni chama ambacho kinafanya maandalizi kwa kizazi kijacho angalia mionombinu ya shule , afya, barabara . mkoa wa singida ni mwiongoni mwa watekelezaji wazuri wa ilani ya ccm .Dkt. Mahenge Amesema wamepokea jumla ya shilingi bilioni tano kwa ajili ya kugharamia ahadi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kuanzia Sabasaba mjini Singida- Sepuka –Ndago-Kizaga yenye urefu wa kilometa 77.
Kama,hiyo haitoshi Desemba 1. 2021 mkuu wa mkoa wa singida Dkt. Binilith Mahenge ameshiriki Utiaji saini Mkataba wa marekebisho ya barabara kwa halmashauri zote Saba (7) za Mkoani hapa kati ya wakala wa barabara za vijijini na mijini TARURA mkoa wa singida na wakandarasi walishinda tuzo ya kazi mkataba wenye thamani ya Sh. Bilioni 12.6.
Utasema
nini juu yaujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya 600 kupitia fedha za mkopo
kutoka IMF kwaajili ya kupunguza athari zitokanazo na ugonjwa wa Uviko 19. Kweli
wanasema wasemaji ‘ Ukinuna uwe na sababu’
‘SEKTA YA AFYA’
Hebu jiulize fedha zilizotengwa za ujenzi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa singida inayojengwa mtaa wa mandewa ambapo sh. Bilioni 5.9 zilizotengwa na ujenzi umefikia asilimia 70 kwa awamu kwanza.uundwaji wa kamati mbalimbali zitakazotekeleza maagizo ya waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt. Doroth Gwajima Kusimamia masuala mbalimbali ikiwemo dawa , uchangiaji Damu matumizi ya fedha .
Tusisahau basi jipya kubwa litakalo wasafirisha wafanyakazi kwenda kuwahudumia wangojwa katika kuboresha huduma. Kutaja machache.
‘KILIMO
NA MAZAO YA KIMKAKATI’
Kupitia
ilani ya chama singida inayo mazao ya kimkakati ambayo lengo lake ni kuokomboa
jamii kiuchumi , mazo hayo ni pamoja na,
i. KOROSHO - Ambapo mkoa umefanikiwa kutekeleza ahadi ya kutoa miche ya mikorosho 202,970. miche 82.008 imepelekwa Halmashauri ya Itigi, na miche mingine 120,962 imepelekwa Halmashauri ya Manyoni.
ii.
ALIZETI- Dk.Mahenge anasema mkoa umeandaa
mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la Alizeti.Ahadi ya utekelezaji huo
utatekelezwa na Halmashauri zote saba kwa kushirikiana na Wizara ya kilimo.Anasema
mkakati huo ni pamoja na kupanua/kuongeza eneo litakalolimwa zao la
alizeti.Jumla ya Ekari 596,909 zitalimwa ikilinganishwa na ekari 205,000 za
msimu wa 2021. Aidha,anasema watahakikisha mbegu bora zinapatikana na kutumika
katika uzalishaji kwa kukidhi mahitaji ambayo kwa mkoa,ni tani 1,194.
iii. KILIMO CHA UMWAGILIAJI - Mkuu huyo wa mkoa,anasema mkoa una jumla ya hekta 2,060.5 zinalimwa kilimo cha umwagiliaji.Pia mkoa una skimu zenye uhakika wa kuhudumia misimu miwili kwa mwaka.
“Tutaendelea
kutoa elimu kwa wakulima 2,036 kati ya 7,039 kuhusu kilimo bora.Vile vile
tutahimiza utunzaji wa miundo mbinu ya umwagiliaji kwenye skimu ya
Itagata-Itigi.Jumla ya ekari 24 zimeongezwa na kufanya jumla ya ekari 219 zenye
miundo mbinu ya maji,”
anasema.
MAPAMBANO DHIDI YA
GONJWA HATARI LA CORONA.
Mkuu
huyo wa mkoa,ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi wenye umri wa kuanzia miaka
18 na kuendelea,wanapata Chanjo ambayo
ni njia yenye ufanisi katika kukinga na kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo.
Anasema
Chanjo ya CORONA inawezesha kinga ya mwili kupambana na virusi vya CORONA pale
mtu anapoambukizwa. Dk.Mahenge anasema Chanjo ya CORONA inatolewa bila malipo
na inapatikana nchi nzima katika Hospitali na Vituo maalum.
Hadi
sasa kupiti wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsis na watoto ,kuna aina nne
za Chanjo ambazo zimeidhinishwa kutumika nchini kwa ajili ya kinga ya CORONA,ambazo ni Johnson and
Johnson,Pfizer,moderna and Sinovac & Sinopharm.
Haya
ni machache kati ya mengi ambayo yanatekelezwa na yataendelea kutekelezwa na
chama hiki kikongwe ambacho kila kada alikulia hapo huwa hatamani kutoka kabisa
, wapo wanaojaribu kwenda kutembea vyama vingine vya upinzani lakini wakiona
matunda na raha wanayoipata hurudi hadi wapinzani hujongea kule kwa wacha
waisome namba eee ccm mbele kwa mbele, mwisho wa siku ‘Utamu wa Kidonda
Hummaliza Inzi’. Asanteni sana Tusherekee kwa amani miaka 60 ya Uhuru wetu .
Kazi iendelee hadi wakati mwingine tena.
0 comments:
Post a Comment