Na Jesca Kishoa, Mbunge
Kwa mujibu wa Global Peace Index kwa nchi za jangwa la Sahara ya mwaka 2020, Tanzania inashika nafasi ya 52 kati ya nchi 163 ikiwa na alama 1.85 chini ya Senegal Botswana, Ghana na Zambia. Mauritius ikiwa nchi ya kwanza yenye amani ikishika nafasi ya 23 ikiwa na alama 1.54 wakati Sudani Kusini ikiwa nchi ya 160 na ya mwisho kwa nchi hizo. Nimeleta mlingano huu ili kuonesha ni kwa jinsi gani amani ni sababu kuu sana kwa kuvutia uwekezaji.
Ripoti ya soko la mafuta na gesi duniani 2021: Madhara ya Uviko-19 na kujikwamua kufikia 2030 imeonesha kuwa itafikia $7425.02 billion ifikapo mwaka 2015, mabadiliko ya 6% kwa mwaka. (CAGR). Hata hivyo, soko hilo hilo kwa mwaka mmoja tu limepanda kutoka $4677.45 billion kwa mwaka 2020, mpaka $5870.13 billion kwa mwaka 2021, ikiwa ni ongezeko la 25.5% (CAGR). Nachohitaji tujue ni sitofahamu hii ya sekta hii duniani ni kuwa inakuwa au inaanguka!
Kutokana na mahitaji ya dunia kwa sasa, jitihada zinachukuliwa katika uwekezaji wa Gesi asilia (LNG). Umoja wa Mataifa pia wameonesha kuihakikishia dunia kwenye kuwekeza rasilimali kwenye nishati hai. Makampuni makubwa duniania yakiwemo ExxonMobil and Shell yameanza kuwekeza kwenye technolojia kama AI na DATA, wakati makampuni mengine kama Chinese Chemical na Petroleum Corporation yakitangaza kuwekeza kwenye intelligent centres takribani 10 zitakazo saidia kupunguza gharama za uendeshaji kwa zaidi ya 20%. Juhudi zimeanza kuchukuliwa ili kuendana na mahitaji ya sasa.
Si kushangaza ni kuwa ripoti hiyo hiyo ya Global Peace Index ilionesha kuwa Msumbiji inashika nafasi ya 99 kati ya nchi 163 za jangwa la sahara ikiwa na alama 2.14. Na kwa kipindi hicho hicho KAMPUNI kubwa ya uwekezaji kwenye mafuta na gesi ikiamua kuondoa mitaji yake inayokadiliwa kuwa $20 billion zilizotegemewa kuwekezwa kwenye mradi wa gesi asilia huko Afungi kufikia 2026. Msumbiji inatakiwa sasa kujiuliza kama itasalia kuwa “jimbo jipya la gesi asilia duniani”, hata hivyo sababu za kiusalama na rushwa zinatajwa kuwa sababu kuu ya kusitishwa kwa uwekezaji huo.
Tofauti na nchi nyingine nilizotaja, ambapo mvutano wa rasilimali umekuwa ukijitokeza, bado kuna msukumo mdogo kwenye kuimarisha amani katika nchi zinazoendelea maana viashia vidogo vidogo hujitokeza na kuondoka hivyo vinahitaji kulitiwa mkazo ili kulinda amani ya nchi hizo. Kama nchi za Africa zinahitaji uwekezaji, basi hazina mbadala wa amani.
Kwa mujibu wa taasisi ya amani ya marekani (United States, Institute of Peace) yenye lengo la kuhakikisha amani inawekana, imeripoti kuwa vitendo visivyo vya kibinadamu huko vinaweza kupelekea makundi hatari kuathiri vya muhimu vinavyoweza kuboresha na kubadilisha kabisa uchumi wa nchi. Kama ilivyotokea kwa wenzetu huko Cabo Delgado, ilipohusishwa na vitendo vya kigaidi.
Tanzania imebahatika kuwa na rasilimali na imebahatika kuwa kuwa ya kimkakati kwenye vyanzo vyake, kwa sababu inakadiliwa kuwa na takribani futi za ujazo trillion 57.54 za gesi asilia iliyovumbuliwa. Tanzania ipo kwenye majadiliano ya kiuwekezaji ukivutia zaidi ya $30 billion kwa ajili ya mradi ya uchakataji wa gesi asilia mkoani Lindi, na inatarajiwa kutoa zaidi ya ajira 15,000 kuanzia 2023 mpaka mradi utakapokamilika 2028. Ninafikiri kuwa huu ni mradi mkubwa sana ambao haujawahi kutokea katika nchi za afrika mashariki na hata kati. Ni mradi utakaochangia ukuaji chanya wa uchumi na taifa letu.
Hivyo, ninashauri yafuatayo:
1. Hili la Msumbiji liwe fundisho wa nchi nyingine ikiwemo Tanzania, tujifunze ku-balance uwepo wa amani na inavyoweza kuvutia uwekezaji, Tanzania imekua nchi ya amani kwa kipindi chote.
2. Majadiliano ya uwekezaji huu wa $30 billion yasiendelee kuchelewa na kama ikiwezekana ujenzi wa mradi uanze ifikapo mwaka 2023 au mapema zaidi kama ikiwezekana. Serikali chini ya Rais Mh. Samia suluhu Hassan iendelee kusimamia na kuilinda amani yetu. Amani ni tunu.
3. Serikali ioneshe utayari na kuwiwa kuharakisha utekelezaji wa mradi huu kwa wakati. Kufanya hivyo, ni fursa inayoweza kuifanya Tanzania kuwa mzalishaji mkuu wa gesi asilia SADC and EAC
4. Gesi asilia mara zote imeonekana kichocheo kikubwa cha uchumi, lakini mara nyingine sababu ya vikwazo na migogoro baina ya mtu mmoja mmoja, vikundi, au serikali kuhusu kunufaika, au kusimamia rasiliamali. Ni vema itumike kwa masilahi ya wengi. Rushwa isipewe nafasi.
5. Muda wote AMANI inahakikishwa na inakuwepo kama wananchi wote wanafaidi matunda ya rasilimali zao, zikielekezwa na kutumiwa vizuri kwa masilahi mapana ya taifa na maendeleo na maisha ya wananchi.
6. Taifa liwekeze rasiliamali kuwe kuimalisha uwepo wa amani muda wote, kijamii, kisiasa, kiuchumi na kisera (tuendelee kuifanya Tanzania mahali salama pa kuwekeza na kuishi)
#AmaniKwaUwekezaji
#VisitTanzania2021
0 comments:
Post a Comment