Mo Dewji |
Mkurugenzi
Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL
Group), Mohammed Dewji amekanusha taarifa ambazo zimesambaa katika
mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa amefanya mahojiano na kituo cha
Redio cha Times FM kuhusu pesa zilizochangishwa katika Tetemeko la Ardhi
la Kagera lililotokea mwezi Septemba, 2016.
Dewji
amesema hajafanya mahojiano na kituo chochote cha habari kuhusu
tetemeko la Kagera na habari hiyo haina ukweli wowote zaidi ni mbinu
ambayo imetumiwa na baadhi ya watu kwa ajili ya kuchafua jina lake na
kampuni yake ya MeTL Group ambayo mpaka sasa ina wafanyakazi zaidi ya
watu 28,000.
Aidha
Dewji amesema ana imani na Serikali ya awamu ya tano na kuwatoa hofu
Watanzania kuwa ataendelea kushirikiana na Serikali kusaidia jamii yenye
uhitaji ikiwa ni sehemu ya ahadi yake ya kutumia nusu ya utajiri wake
kusaidia watu wenye uhitaji.
“Nitumie
nafasi hii kuwajulisha Watanzania wenzangu kuwa hii habari ambayo
inasambazwa na watu katika mitandao ni ya uongo na haina ukweli wowote,
sijafanya mazungumzo na media yoyote na mimi nilichangia pesa kwa nia
nzuri, nina imani na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk.
John Magufuli kuwa inafanya kazi kwa faida ya watu wote bila kufanya
ubaguzi,” amesema Dewji.
0 comments:
Post a Comment