METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, September 11, 2021

VIJANA 60 WAPATA MAFUNZO YA TEHAMA

Baadhi ya vijana waliohitimu mafunzo ya Tehama wakifurahia jambo wakiwa na mratibu na mkufunzi wa mafunzo ya TEHAMA kitengo cha kompyuta kutoka chuo kikuu cha Dar Es Salaam, Jesca Tesha aliyevaa Ngauni la njano.

Baadhi ya wanafunzi wa  Tehama wakiwa darasani wakipata mafunzo kwa vitendo

Baadhi ya wanafunzi wa  Tehama wakiwa darasani wakipata mafunzo kwa vitendo.

Baadhi ya wanafunzi wa  Tehama wakiwa darasani wakipata mafunzo kwa vitendo

Jumla ya vijana 60 wamehitimu mafunzo ya Mawasiliano na Teknojia ya Habari –TEHAMA katika kanisa la Aict-Kitete klasta ya Tabora mafunzo yaliyodhaminiwa na shirika la Compasion Internatinal Tanzania.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo hayo kiongozi wa klasta ya Tabora Huduma ya maendeleo ya mtoto na kijana, Emmanuel Russota amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwakomboa vijana kutoka kwenye umaskini wa kiroho na kimwili.

Alisema kwamba lengo ni  kumkomboa kijana kutoka kwenye umasikin wa kiroho,kiakili na kijamii na kuleta ukamilifu wa maisha ya binadamu ili  kuweza kurahisisha maisha au kuweza kumfanya kila mwanadamu aweze kuishi maisha Kama binadamu wengine walivyoweza kufanikiwa

Alisema kwamba mafunzo haya ni sehemu ya utekelezaji wa elimu ya digital literacy promotion skills ambayo inamjenga kijana kuweza kupata uwezo wa kutengeneza kuwa mtaalum wa Tehama

Kwa upande wake mratibu na mkufunzi wa mafunzo ya TEHAMA kitengo cha kompyuta kutoka chuo kikuu cha Dar Es Salaam, Jesca Tesha amewaka vijana hao kuyazingatia yale waliyojifunza kwa muda wa wiki mbili.

Alisema kwamba mafunzo hayo yanaweza kutoa kijana kwenye umasikini na kumuongezea maafifa ya kukuza uchumi wake na familia na Taifa kwa jumla

Naye afisa maendeleo ya jamii kata ya Kitete Wahabi Waziri  alisema shirika la Compasion Internatinal Tanzania limetumia pesa nyingi kugharamia mafunzo hayo hivyo vijana hao wanapaswa kuendeleza yale waliyojifunza. 

Alisema kwamba licha  shirika la Compasion Internatinal Tanzania kutoa fedha lakini limewekeza kwa vijana ambao ndio Taifa la kesho ambapo wamepata dira na muelekeo wa maisha yao ya baadaye  

Nao baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo Protas Malenge na Jackline Gwadenga walisema wamejifunza mambo mbalimbali kwa muda wa wiki mbili na kwamba imewaongezea ujuzi katika maisha yao hasa kwenye.  

Huduma ya maendeleo ya mtoto na kijana inahusisha makanisa 11 yanayoshirikiana na shirika la Compasion Internatinal Tanzania yenye lengo la kumkomboa mtoto au kijana kutoka kwenye umaskini.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com