METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, August 25, 2021

WAZIRI MKENDA AMUHAKIKISHIA MKUU WA MKOA WA SINGIDA UPATIKANAJI WA MBEGU BORA ZA ALIZETI

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Bilinith Mahenge, Uongozi wa Wilaya za mkoa huo pamoja na wataalamu wote wa kilimo kutoka Wizara ya Kilimo ili kujadili upatikanaji wa mbegu za alizeti, Leo tarehe 25 Agosti 2021 Jijini Dar es salaam.(Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Bilinith Mahenge, Uongozi wa Wilaya za mkoa huo pamoja na wataalamu wa kilimo kutoka Wizara ya Kilimo ili kujadili upatikanaji wa mbegu za alizeti, Leo tarehe 25 Agosti 2021 Jijini Dae es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Bilinith Mahenge akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi na wataalamu wa kilimo wakiongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda ili kujadili upatikanaji wa mbegu za alizeti, Leo tarehe 25 Agosti 2021 Jijini Dae es salaam.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Bilinith Mahenge kabla ya mkutano wa kujadili upatikanaji wa mbegu za alizeti, Leo tarehe 25 Agosti 2021 Jijini Dae es salaam.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Bilinith Mahenge, Uongozi wa Wilaya za mkoa huo pamoja na wataalamu wote wa kilimo kwa kuitikia wito wa serikali wa kutekeleza matakwa ya serikali katika kukabiliana na upungufu wa mafuta ya kula.

 

Waziri Mkenda ametoa pongezi hizo leo tarehe 25 Agosti 2021 katika Ofisi za Wizara ya Kilimo zilizopo katika mtaa wa Tazara Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida akiwa ameambatana na wataalamu wa Kilimo.

 

Waziri Mkenda amesema kuwa pamoja na mikoa yote kuitikia wito huo wa serikali katika kuongeza tija na uzalishaji wa alizeti ili kukabiliana na upungufu wa mafuta ya kula kiasi kuagiza mafuta nje ya nchi, mkoa huo wa Singida umeibuka na mkakati kabambe ili kutekeleza maelekezo hayo ya serikali.

 

“Na wewe mkuu wa mkoa huna makeke lakini mambo yako yanaonekana sana, na mimi nipende kukuahidi kuwa serikali inaendelea na mkakati wa kuimarisha upatikanaji wa mbegu za alizeti ili kuwa na mbegu bora na za kutosha“ Amekaririwa Waziri Mkenda

 

Waziri Mkenda ametoa wito kwa wakulima wakubwa kuhakikisha kuwa wanaingia mkataba na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa mbegu pamoja na masoko.

 

Kadhalika amewasihi wakulima wadogo kuhakikisha kuwa wanaingia mikataba na Taasisi za serikali kupitia Vyama Vya Msingi Vya wakulima ili kurahisisha huduma hiyo ya upatikanaji wa mbegu bora na masoko ya uhakika.

 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Bilinith Mahenge amesema kuwa mkoa huo upo katika utayari mkubwa kwa ajili ya kilimo cha alizeti kwani una ardhi ya kutosha na isiyokuwa na migogoro kama ilivyo katika mikoa mingine nchini.

 

Amesema kuwa kwa kuanzia tayari mkoa huo umetenga Hekari 596,000 kwa ajili ya kilimo cha alizeti huku akitoa wito kwa serikali kuhakikisha mbegu zinapatiakana kwa wakati kwani jambo hilo likifanyika kwa wakati itakuwa ni chachu kwa wakulima kuongeza ukubwa wa maeneo yao ya kilimo.

 

MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com