Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu
“Tija ya zao la pamba kwa sasa ni kilo 200 hadi 300 kwa ekari. Taarifa nilizonazo, tunaowakulima wanozingatia kanuni 10 za kilimo bora cha pamba na tija yao ni kati ya kilo 1,000 na 1,200 kwa ekari. Tanzania ina fursa kubwa ya kuongeza uzalishaji wa pamba kutoka wastani wa tani 300,000 hadi tani 1,000,000”
Waziri
wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo tarehe 5 Julai 2021 wakati Akizindua kampeni ya Kuongeza Tija
katika zao la Pamba iliyofanyika Kijiji cha Kijereshi Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.
“Kwa
lengo la kufikia lengo la kuzalisha tani 1,000,000 ifikapo mwaka 2025 kama
ilivyoainishwa kwenye ilani, leo ni siku muhimu sana. Nimezindua kampeni ya
kuongeza tija katika zao la pamba. Wizara iliona ni muhimu kuendesha kampeni
kabambe ya kuwahamasisha wakulima wa pamba kuzingatia kanuni 10 za kilimo bora
cha pamba” Amekaririwa Waziri Mkenda
Amesema
Kwa kuwa pamba inazalishwa katika Mikoa 17 nchini, hivyo Wakuu wa Mikoa na
viongozi wote katika ngazi mbalimbali, wanapaswa kuunga mkono juhudi hizo
ikiwemo Wabunge kusaidia kuelimisha wananchi katika maeneo yao ili kilimo cha
pamba kiwe mkombozi wa maisha wakulima na watanzania kwa ujumla wake.
Waziri
Mkenda amesema kuwa kilimo kinakabiliwa na tatizo kubwa la tija kuwa ndogo sana
karibu katika kila zao. Hali hiyo inasababisha pato la mkulima kuwa chini.
”Wizara
yangu imelitambua tatizo hili la msingi na kwamba tuna jukumu kwanza la
kuuelimisha umma na wakulima kwa ujumla juu ya umuhimu wa kuangalia pato la
mkulima kama kigezo cha ufanisi katika shughuli zote za kilimo. Pili tuna
wajibu wa kuweka mazingira sahihi ili kila mkulima nchini wa zao lolote abadili
maisha yake kutokana na shughuli yake. Hivyo, kwa nafasi ya pekee niwapongeze
Wadau wa Pamba kuwa wa kwanza kutekeleza maono ya Wizara ya Kilimo katika kuongeza
tija” Amesema Waziri Mkenda
Waziri
wa Kilimo amesem akuwa Kipato cha mkulima kinategemea kiasi mkulima
anachozalisha kwa ekari, ubora wa zao na bei ambayo soko liko tayari kulipa.
Mkulima yoyote ana uwezo wa kupata tija kubwa na kuzalisha zao bora. “Muda
umefika wa viongozi na wakulima kuelewa kwamba tija ikiwa kubwa kwa bei yoyote
itakayokuwepo sokoni, pato litakuwa kubwa” Amesisitiza
Waziri
Mkenda amesema kuwa ili kilimo kiweze kutoka kwenye tija ndogo, suala la
kuboresha utoaji wa huduma za ugani ni la lazima. Katika mwaka huu wa fedha jumla
ya Pikipiki 1,500 zitanunuliwa na kusambazwa katika mikoa mbalimbali baada ya
kutosheleza Mikoa ya Dodoma, Singida na Dodoma.
Amesema
kuwa kuwa Lengo ni kufanya vizuri katika Mikoa 3 ili mwaka ujao kujipima kiasi
cha mafanikio na kuongeza nguvu kuifikia mikoa mingine; ikiwa ni pamoja na Maafisa
Ugani kupatiwa mafuta ili kuwawezesha
kutekeleza majukumu yao; na Ili kuimarisha usimamizi vyombo vya usafiri vitafungiwa
GPS.
Kwa
upande wake Balozi wa Pamba Tanzania Ndg Aggrey Mwanri akizungumza wakati wa
uzinduzi huo amesema kuwa ili tija iweze kuongezeka kwenye zao la Pamba ni
lazima wakulima Kubadili vipimo vya kupandia kutoka 90x40cm na kuwa 60x30cm
ambapo idadi ya mimea kwa ekari itaongezeka kutoka 22,222 hadi 44,400.
Mabadiliko yanafanyika baada ya kukamilika kwa utafiti uliofanywa na TARI
Ukiriguru na kuonesha ongezeko kubwa la tija kufikia kilo 1,000 kwa ekari.
Mwanri
amesema kuwa wakulima wanapaswa Kusomba samadi na kusambazwa mashambani ili
kurutubisha udongo ambapo wakulima wa pamba wanapaswa kuondokana na matumizi ya
jembe la palizi la kukokotwa na wanyamakazi. Hatua hii itarahisisha palizi
kufanyika kwa saa 2 kwa ekari badala ya siku 7 kwa jembe la mkono;
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Ndg Marco Mtunga amesema kuwa Bodi ya Pamba
imejipanga Kuimarisha huduma za ugani, Kusambaza kamba za kupandia katika
wilaya zote ili kuwezesha wakulima wa pamba kuzingatia vipimo vipya vya
upandaji; na Pembejeo zote ikiwemo mbegu, viuadudu, vinyunyizi kusambazwa kwa
wakati.
Ameongeza
kuwa katika maeneo yote ya usukumani na mikoa inayolima Pamba wakulima hawana
tatizo la nguvu kinachokosekana ni maarifa machache yanayopatikana kwenye
kilimo cha Pamba.
Hata
hivyo amewapongeza wakulima wa Pamba kote nchini kwa kuitikia mwito wa serikali
wa kuhakikisha uzalishaji unaongezeka katika msimu wa mwaka 2020/2021 hivyo
amewaomba wananchi kuitikia tena mwito wa serikali kuhakikisha kuwa uzalishaji
na tija unazidi kuongezeka.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment