METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, July 14, 2021

NAIBU MWANAIDI AAGIZA KUANZISHWA KWA VITUO VYA HUDUMA ZA PAMOJA (ONE STOP CENTRE) KUPAMBANA NA UKATILI

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Mahakama ya Hakimu Mfawidhi, Kigoma alipotembelea Mahakama hiyo kuona namna ya uendeshaji wa mashauri yanayowahusisha watoto. Walioketi kulia ni Hakimu mfawidhi Gadiel Marik na kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Simon Chacha 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis akitazama moja ya mashuka yanayofumwa na wanakikundi cha Wanawake wa Upendo (Upendo Women Group) kilichopo Kata ya Mwanga Kaskazini, Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma. 

Wanawake wa Kikundi cha Upendo women Group wakimkabidhi zawadi ya Shuka Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis alipofika katika  Kata Mwanga Kaskazini, Manispaa ya Kigoma Ujiji kuona kazi zinazoendeshwa na wanawake hao kutokana na Mkopo wa asilimia nne zinazotokana na mapato ya Halmashauri.

Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis ameagiza kuanzishwa kwa vituo vya huduma ya pamoja kwa waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto ili kuwezesha kusikilizwa kwa mashauri hayo na kuharakisha utoaji wa haki.

Naibu Waziri Mwanaidi ametoa agizo hilo Mkoani Kigoma mara baada ya kutembelea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma na kupata taarifa za uendeshaji wa mashauri ya ukatili dhidi ya watoto pamoja na changamoto zinazowakabili watendaji wa mahakama hiyo.

Amesema pamoja na jitihada zilizopo za kuanzisha vituo vya huduma kwa wahanga wa ukatili kwa pamoja, jitihada zaidi zinahitaji kwa kushirikiana na Serikali ili kupunguza au kumaliza kabisa vitendo vya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto.

Hata hivyo, amewashukuru wadau wa maendeleo wanaoshughulika na mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa kuanzishaji wa vituo vya mkono kwa mkono ikiwa ni jitihada za kuhakikisha kwamba vitendo vya ukatili vinatokomezwa.

Awali akitoa taarifa kwa Naibu Waziri Mwanaidi, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Gadiel Marik amesema Mhakama imekusanya maoni ya wadau kuhusu haki jinai kwa ajili ya kusikiliza katika mahakama za waoto

Baadhi ya watendaji katika mahakama hiyo wamependekeza kuboreshwa kwa huduma kwa kuanzishwa kwa vituo vya pamoja na kuboresha vitendea kazi.

Aidha, Naibu Waziri Mwanaidi ametembelea vikundi mbalimbali vya wajasriamali kwa lengo la kuona jinsi wanavyonufaika na mkopo wa asilimia 10, asilimia 4 kwa wanawake, 4 kwa vijana na asilimia 2 kwa wenye ulemavu kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com