Katibu Mkuu Ndugu Daniel
Chongolo amekutana na kuzungumza na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mzee Pius
Msekwa katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu Lumumba na kumuahidi kukitumikia,
kukisimamia na kukiimarisha zaidi Chama Cha Mapinduzi.
Chongolo amemhakikishia
Mzee Msekwa kuwa Chama kipo salama chini ya Sekreterieti anayoiongoza na kwamba
Katiba, Kanuni, taratibu na miongozo ya Chama iliyowekwa na Waasisi wa CCM
itaendelea kuheshimiwa, kulindwa na kufuatwa, na kwamba Jahazi la CCM chini ya
uongozi wake halitakwenda mrama.
Katibu Mkuu mpya wa CCM
ameeleza kuwa mafunzo ya uongozi, utawala na siasa aliyoyapata wakati wote
akiwa mtumishi kwenye Chama na Serikalini yamemkomaza na kumuandaa vyema kwa
nafasi aliyoteuliwa na Mwenyekiti wa CCM Ndugu Samia Sukuhu Hassan.
Chongolo amemueleza Mzee Msekwa kuwa amejifunza mengi kutoka kwa Wazee wastaafu
aliobahatika kufanya kazi chini yao, amejifunza Ujasiri, kujiamini na kupata
upeo na maarifa ya kutosha.
"Nakushukuru sana
Mzee Msekwa, wewe na viongozi wenzako wastaafu kwa jinsi mlivyonilea. Nimechota
maarifa na kujifunza mengi kutoka kwenu na kuniandaa. Nichukue nafasi hii
kukuhakikishia kwa fikra zile zile, nidhamu ile ile na misimamo
inayozingatia mabadiliko ya nyakati CCM kitaendelea kubaki chama bora
Barani Afrika "Alisema Chongolo.
Ndugu Chongolo amesema
licha ya kujifunza na kupata uzoefu wa kutosha ataendelea kujifunza zaidi.
Amesema kila atakapokwama hatosita kukimbilia kwao kwa ushauri na elimu ya
uongozi.
Kwa upande wake Mzee
Msekwa alisema CCM hakijawahi kumkabidhi mwanachama wake yeyote dhamana ya
kuongoza hata ofisi ya tawi ikiwa mtu au mwanachama huyo hatoshi na hana
vigezo. Hivyo akamuhakikishia Ndugu Chongolo kuwa Mwenyekiti wa CCM na wajumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa wamejiridhisha kuwa anatosha, akamshauri aonyeshe
utiifu, nidhamu na kukisimamia chama kwa uamunifu na kupokea na kuzingatia
maelekezo atakayopewa na Mwenyekiti na Vikao vya Chama.
"Una wajibu
wa kuhakikisha Sekreterieti yako muda wote mnakuwa na msimamo wa pamoja.
Una kazi ya kutekeleza maagizo aidha ya H/kuu ya Taifa au ya Kamati Kuu ya CCM
na kutekeleza" Alisema Mzee Msekwa.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment