METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, February 4, 2021

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUNGUA MAJENGO YA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA PAMOJA NA MIRADI MINGINE YA JESHI HILO MKOANI DODOMA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene wakati akizindua nyumba za makazi ya Maafisa na Askari Magereza katika eneo la Gereza la Isanga mkoani Dodoma leo tarehe 04 Januari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene, Kamishna Jenerali wa Magereza CGP Suleiman Mzee pamoja na baadhi ya Viongozi Wakuu vya Vyombo vya Ulinzi na Usalama, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa nyumba 24 za makazi ya Maafisa na Askari Magereza katika eneo la Gereza la Isanga mkoani Dodoma leo tarehe 04 Januari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua nyumba hizo za mpya za Maafisa na Askari Magereza katika eneo la Gereza la Isanga mkoani Dodoma leo tarehe 04 Januari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mhandisi Bonanza Marata kuhusu mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha Samani cha Jeshi la Magereza mkoani Dodoma kabla ya kuweka jiwe la msingi leo tarehe 04 Januari 2021 katika eneo la Msalato. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene wakati  akiweka jiwe la Msingi ujenzi wa Kiwanda cha Samani cha Jeshi la Magereza Msalato mkoani Dodoma. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua baadhi ya Mashine ambazo zimeanza kufungwa katika Kiwanda hicho cha Samani cha Magereza. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine wakati akifungua Majengo ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Msalato mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ofisi ya Kamishna Jenerali wa Magereza CGP Suleiman Mzee mara baada ya kufungua Majengo ya Makao Makuu ya Jeshi hilo Msalato mkoani Dodoma. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene wakati akielekea kuhutubia wananchi Msalato mkoani Dodoma. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Maafisa na Askari Magereza mara baada ya kufungua Majengo ya Makao Makuu ya Jeshi hilo Msalato mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua na Kuendesha magari mapya ya Jeshi la Magereza nchini mara baada ya kufungua Majengo ya Makao Makuu ya Jeshi hilo Msalato mkoani Dodoma.  Taaswira ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza yaliyopo Msalato mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com