METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, October 6, 2020

MILIONI 105 ZAKOPESHWA BUSWELU KUWAKOMBOA WANANCHI KIUCHUMI

Kiasi cha shilingi milioni 105 kutoka halmashauri ya manispaa ya Ilemela zimekopeshwa kwa wananchi wa kata ya Buswelu waliojiunga katika vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili waweze kuanzisha shughuli za uzalishaji mali na kujikomboa kiuchumi.

Hayo yamebainishwa na mgombea ubunge wa jimbo la Ilemela kupitia Chama Cha Mapinduzi Ndugu Dkt Angeline Mabula wakati akizungumza na maelfu ya wananchi wa kata ya Buswelu katika viwanja vya Bujingwa senta waliojitokeza kumsikiliza katika muendelezo wa mikutano yake ya kampeni kuomba kuchaguliwa tena kuwa mbunge wa jimbo hilo ambapo amesema kuwa Serikali ya CCM chini ya Rais Mhe Dkt John Magufuli imetunga sheria ya fedha ya mwaka 2020 inayozielekeza halmashauri zote nchini kutenga asilimia kumi za mapato yake ya ndani kwaajili ya kukopesha vikundi vya wajasiriamali vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili waweze kukuza mtaji wa shughuli za uzalishaji mali wanazozitekeleza na kujikomboa kiuchumi

‘.. Mapato yetu ya ndani yameongezeka maana yake na uwezo wa kukopoesha watu wetu unaongezeka, Niwaombe vijana jitokezeni kutumia fursa hii kujikwamua kiuchumi, kupunguza changamoto ya ajira ..’ Alisema

Aidha Dkt Mabula akawaasa vijana kuwa waaminifu  kwa kuhakikisha wanarejesha fedha wanazokopeshwa ili vijana wengine waweze kukopa pia kuzitumia kwa malengo yaliyojikusudiwa kwa kuanzisha miradi ya kimaendeleo.

Akimkaribisha mgombea huyo, Meneja kampeni Ndugu Kazungu Safari Idebe akawaomba wananchi hao kuendelea kukiamini chama cha mapinduzi na kukichagua tena katika uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba 28, mwaka huu ili utekelezaji wa shughuli za maendeleo uweze kuendelea.

Akihitimisha katibu wa CCM wilaya ya Ilemela Bi Aziza Isimbula akawaomba wananchi wa kata ya Buswelu kuchagua wagombea wa nafasi ya uraisi, ubunge na udiwani kutoka chama cha mapinduzi kwani wanyo Ilani ya uchaguzi iliyobeba mahitaji yao na inayoweza kutekelezeka.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com