Wakulima wa zao la Korosho Kijiji cha Tingi Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi Wakiskiliza Maelekezo ya Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga.
Na Innocent Natai, Lindi
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga awataka
Wakulima kuachana na Kilimo cha kutegemea Mvua na badala yake kutumia maji ya Mito
na Mabwawa kwa kufanya Kilimo cha umwagiliaji ili kuwasaidia kuondoakana na changamoto ya upungufu wa mvua kwani ndio njia itakayo wawezesha Kulima Kilimo chenje tija.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na
wakulima wa zao la Korosho katika Kijiji cha Tingi,
Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi wakati akiendelea na ziara yake kwa siku ya pili
ya kusikiliza na kutatua kero na changamoto zinazowakabili wakulima wa zao la Korosho.
Hasunga amesema suala la Upungufu wa mvua limekuwa likitumiwa na wakulima kama sababu inayopelekea ukosefu wa mazao ya kutosha hivyo ni vyema sasa wakajikita katika matumizi ya maji ya Mito na Mabwawa katika Kilimo kwani mbali na kuondoa changamoto ya upungufu wa maji pia itawawezesha kuondokana na Kilimo cha msimu kisichikuwa na tija hivyo wataweza Kulima kwa kipindi kirefu bila ya kupumzika huku wakinufaika na Kilimo hicho.
Amewataka wakazi wa Kilwa kutumia vizuri Bonde
la mto Rufiji kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo
kwani ni eneo lenye maji ya kutosha kwa ajili ya umwagiliaji na lenye rutuba ya
kutosha kwa ajili ya Kilimo.
“Bonde la mto Rufiji likitumika ipaswavyo
lina uwezo wa kuzalisha chakula cha kutosha kwa mwaka mzima lakini kwa sasa
halitumiki ipaswavyo ni mapori tu yamejaa” Amesema
Aidha, amesema kuwa serikali kupitia Wizara ya Kilimo imedhamiria kuhakikisha inatumia fursa ya uwepo wa Mradi wa kufua umeme unaotokana na maporomoko ya maji ya Mto Rufiji maarufu kama Stiglers.
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga anatarajiwa kumaliza ziara yake ya Siku tatu ya kutembelea, kuskiliza na kutatua kero zinazowakabili Wakulima wa zao la Korosho katika baadhi ya Wilaya za Mikoa ya Pwani na Lindi ambapo leo atahudhuria Mkutano wa Wadau wa Korosho utakaofanyikia Mkoani Lindi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment