Katibu Mkuu
Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya mapema leo tarehe 12 Agosti, 2020
amewapongeza Viongozi na Wafanyakazi wa kiwanda cha sukari Kagera kwa
kutanguliza maslai ya taifa mbele kwa kuongeza eneo la kilimo cha miwa kiasi
cha hekta elfu 16 (16,000) ambapo uzalishaji unatarajiwa kufika kiasi cha tani
170,000.
Katibu Mkuu
amesema hatua hiyo ni ya kujivunia kama nchi kwa kuwa Taifa limekuwa likipitia
changamoto ya kukosa sukari katika kipindi cha mwezi Machi hadi Mei kila mwaka;
kutokana na viwanda vyote vinne vinavyozalisha sukari nchini kusimamisha
uzalishaji kwa kuwa huo si wakati mzuri wa kilimo cha miwa kutokana sababu ya
mvua za masika.
Katibu Mkuu
ameongeza kuwa mahitaji ya sukari nchini kiasi cha tani 470,000 wakati
uzalishaji wetu ufikia tani 359,000.
“Nawapongeza
kiwanda cha Kagera sukari kwani baada ya uapnuzi wa kiwanda pamoja na
kuongezeka kwa eneo la kilimo la hekta 16,000 kuanzia mwaka 2024/25 taifa
litapata ziada ya tani 170,000.” Amekaririwa Katibu Mkuu Kusaya.
0 comments:
Post a Comment