Kaimu
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii
Bi. Ruth Minja akieleza kwa waandishi leo Julai 8, 2020 wa
habari kuhusu mfumuko wa Bei kwa mwezi June 2020 ambao
umeendelea kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa mwezi Mei, 2020.
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa kutangaza mfumuko wa bei
kwa mwezi June, 2020 Jijini Dodoma leo
Julai 8, 2020.
Mfumuko
wa bei wa Taifa kwa mwezi Juni 2020
umeendelea kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa mwezi Mei, 2020.
Akizungumza
leo Julai 8, 2020 Jijini Dodoma, Kaimu
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS), Bi. Ruth Minja amesema kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya
mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka unaoishia mwezi Juni umebaki
kuwa sawa na iliyokuwepo kwa mwezi Mei.
Akifafanua,
Bi Minja amesema kuwa baadhi ya bidhaa za vyakula zilipungua bei kwa mwezi Juni
2020 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2019, baadhi ya bidhaa hizo ni
pamoja unga wa mahindi kwa asilimia 1.6, matunda kwa asilimia 2.1, viazi
mviringo asilimia 0.5 na mihogo asilimia 13.3.
Kwa
upande wa bidhaa zisizo za vyakula amesema kuwa ziliongezeka bei kwa mwezi
Juni, 2020 ikilinganishwa na bei za mwezi Juni 2019, bidhaa hizo ni pamoja na
mavazi kwa asilimia 2.7, gesi ya kupikia kwa asilimia 7.8 , mkaa asilimia 11.2,
samani asilimia 2.7 na vitabu vya shule kwa asilimia 1.5.
Mfumuko
wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Juni,
2020 umepungua hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 4.4 kwa mwaka unaoishia mwezi
Mei, 2020.
Kwa
upande wa nchi ya Kenya Bi Minja amesema kuwa Mfumuko wa bei kwa mwaka
ulioishia mwezi Juni, 2020 umepungua hadi kufikia asilimia 4.59 kwa mwaka
ulioishia mwezi Mei, 2020. Kwa upande wa Uganda, Mfumuko wa bei kwa mwaka
ulioishia mwezi Juni, 2020 umeongezeka hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 2.8
kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2020.
0 comments:
Post a Comment