Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akiangalia kichomeo cha kinachotumika kuteketeza mifuko isiyokidhi viwango vya okea sehemu ya mifuko isiyokidhi viwango iliyokamatwa katika mikoa ya Tabora, Singida na Dodoma na kuteketezwa katika kichomeo cha kisasa katika Hospitali ya Mt. Gaspar iliyopo Halmashauri ya Itigi, Wilaya ya Manyoni, Mkoa wa Singida.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Mussa Azzan Zungu akizungumza kabla ya kushuhudia zoezi la uteketezaji wa shehena ya mifuko isiyokidhi viwango. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Rahabu Solomon, kushoto ni Meneja wa Kanda ya Kati wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Novatus Mushi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Mussa Azzan Zungu akitembelea wafanyabiashara na wananchi kuwahamasisha matumizi ya mifuko mbadala inayokidhi viwango katika maeneo ya Halmashauri ya Itigi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa wazalishaji na wasambazaji wa mifuko isiyokidhi viwango ili kudhibiti uchafuzi utokanao na mifuko hiyo.
Zungu alitoa kauli hiyo Itigi Wilayani Manyoni mkoani Singida leo baada ya kushuhudia zoezi la uteketezaji wa zaidi ya tani 11.53 za mifuko mbadala aina ya non-woven iliyokamatwa katika mikoa ya Tabora, Singida na Dodoma.
Katika zoezi hilo lililofanyika kwa kutumia kichomeo taka cha kisasa cha Hospitali ya Mt. Gaspar iliyopo wilayani humo aliwataka wananchi kutonunua mifuko isiyokidhidhi viwango vya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kufanya hivyo watengenezaji hawatapata soko na hivyo itaisha.
“Mifuko hii ni michafu na inaharibu mazingira, Serikali imeshatoa agizo na sheria imetungwa lakini mifuko hii inarudi hapa wafanyabiashara wana kiburi wanadharau mamlaka na sisi tutachukua hatua stahiki, lakini tutaendelea kutoa elimiu kwa wananchi” alisisitiza Zungu.
Alitoa rai kwa wazalishaji, wasambazaji na wananchi kwa ujumla kuwa ni kosa kisheria kutumia mifuko aina ya non-woven isiyokidhi viwango vya ubora na hatutasita kuchukua hatua kwa mtu yeyote au kiwanda kitakachozalisha mifuko mbadala isiyokidhi viwango vya ubora.
0 comments:
Post a Comment