Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akikagua ramani wakati wa kutatua
mgogoro wa Ardhi baina ya Kijiji cha Nanyala na kiwanda cha Saruji cha
Mbeya, Waziri Lukuvi aliambatana na Ma naibu waziri wa Wizara za
Tamisemi, Madini na Viwanda na Biashara.
Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiambatana na Ma naibu waziri wa
Wizara za Tamisemi, Madini na Viwanda na Biashara kukagua eneo lenye
Mgogoro kati ya Kijiji cha Nanyala Wilaya ya Mbozi na Kiwanda cha Saruji
cha Mbeya.
Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi eneo linalotumika kuchimba madini ya
Marumaru ambalo pia liko kwenye mgogoro wa Ardhi baina yao na kiwanda
cha Saruji cha Mbeya, Waziri Lukuvi aliambatana na Ma naibu waziri wa
Wizara za Tamisemi, Madini na Viwanda na Biashara.
Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, Naibu Waziri Viwanda na Biashara
Mhandisi Stella Manyanya(kushoto), Naibu Waziri Madini Stanlaus Nyongo
na Naibu Waziri OR TAMISEMI Josephat Kandege wakisikiliza maelezo kuhusu
mgogoro wa ardhi baina ya Kiwanda cha Saruji cha Mbeya na Kijiji cha
Nanyala cha Wilaya ya Mbozi.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela (aliyevaa kofia), akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Albert Chalamila na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William
Lukuvi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kutatua mgogoro wa ardhi kati
ya kiwanda cha Saruji cha Mbeya na Kijiji cha Nanyala.
***********************************
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliagiza Wizara za
Ardhi, Madini, Tamisemi na Viwanda zishughulikie mgogoro wa Ardhi baina
ya Kijiji cha Nanyala na kiwanda cha Saruji cha Mbeya.
Mgogoro unahusisha ekari 2315 ambapo ekari 1475 zipo Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe na ekari 840 ziko wilaya ya Mbeya.
Leo tumekuja kama
alivyoagizwa kujionea hali halisi ikiwa lengo letu ni kuumaliza mgogoro
huo na tutafuata sheria taratibu na kanuni zote katika kutatua mgogoro
huu.
Kufikia Jumatatu
Kiwanda cha Saruji kiondoe kesi tatu zilizoko mahakamani baina ya
kiwanda na wana kijiji cha Nanyala kama alivyo agiza Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, hii si hiyari, haiwezekani
Mkuu wa Nchi anaagiza jambo halafu kuna mtu anajivuta kutekeleza.
Utoaji wa leseni
za madini katika eneo lenye mgogoro usitishwe, Kijiji cha Nanyala,
Wilaya za Mbozi na Mbeya zisitishe utoaji wa hati za kimila katika eneo
lenye mgogoro.
Wakulima na
wafugaji ambao wanalima na kufuga katika eneo hilo, mgogoro huu hauna
maslahi nao hivyo wasizuiliwe kuendelea na shughuli za kilimo na
ufugaji.
Wachimbaji wadogo
wadogo wa chokaa wanaofanya shughuli zao kwa msimu katika eneo lenye
mgogoro wasizuiliwe waendelee kufanya kazi zao.
Naibu Waziri Madini Stanslaus Nyongo
Wataalamu
waangalie namna ya kubalidisha Sheria ya Service Levy ili halmashauri za
Mbeya na Mbozi waweze kufaidika kwa pamoja na sio halmashauri moja
kufaidika huku nyingine ikipunjwa.
Kiwanda cha
Saruji cha Mbeya kama wanataka kutunza eneo kwa ajili ya matumizi ya
baadaye waangalie namna bora inayotambulika kisheria na sio kukwepa
gharama kwa kutofuata taratibu na sheria.
Naibu Waziri OR TAMISEMI Josephat Kandenge
Halmashauri
ambayo haikupata service levy na ilistahili kupata ilipwe kwakuwa
tusirekebishe ya mbele bila kuangalia stahiki zilizopita za Halmashauri
hizi.
Naibu Waziri Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya
Wizara ya Viwanda
na Biashara ingependa kuona mgogoro huu unaisha kwakuwa kiwanda cha
Saruji na vingine vilivyopo katika eneo hilo vina mchango katika
maendeleo ya taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila
Migogoro
inapoendelea sana lazima kuna upande unakuwa hauna uelewa hivyo
wataalamu watusaidie katika hilo pia tusiingie sana katika mgogoro wa
mapato kuwa yaende kwa nani isipokuwa tujielekeze kuumaliza mgogoro huo.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela
Mkoa wa Songwe tunaomba kesi zifutwe ili wananchi waendelee kufanya shughuli zao kwa uhuru.
Mkoa wa Songwe
tunataka wawekezaji na tunawakaribisha waje kwakuwa sisi tuna mali ghafi
za kutosha ila tu wajue kuwa lazima sheria na taratibu zifuatwe.
0 comments:
Post a Comment