Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard
Kalemani pamoja na Mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde
awakitia saini kwenye daftari la wageni leo walipokuwa wakiwasha umeme
katika hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa
Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Afisa Tarafa ya Makanjwa Bi.Anifa
Byemelwa,akimkarisha Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard Kalemani,ambaye
leo ameweza kuwasha umeme katika hospitali ya wilaya ya chamwino
iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Diwani Kata ya Mlowa Barabarani
Bw.Allan Matewa,akizungumza mbele ya Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard
Kalemani,ambaye leo amewasha umeme katika hospitali ya wilaya ya
chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Meneja Tanesco wilaya ya Chamwino
Bw.Baltazar Massawe,akitoa taarifa ya usambazaji umeme wilayani humo kwa
Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani,alipokuwa ameenda kuwasha umeme
katika hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa
Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino
Mhe.Vumilia Nyamoga,akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nishati
Mhe.Dkt.Medard Kalemani,ambaye amewasha umeme katika hospitali ya
wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo
jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard
Kalemani,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mlowa Barabarani wakati
wa kuwasha umeme katika hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa
kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Mtera Mh.
Livingstone Lusinde akiwahutubia wananchi wa jimbo lake katika kijiji
cha Mlowa Barabarani ambapo Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard
Kalemani,leo amewasha umeme katika hospitali ya wilaya ya chamwino
iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Sehemu ya jengo la hospitali ya
wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo
jijini Dodoma ambayo leo imepata umeme.
Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard
Kalemani,akisisitiza jambo kwa wananchi wa kijiji cha Mlowa Barabarani
kabla ya kuwasha umeme katika hospitali ya wilaya ya chamwino
iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard
Kalemani,akitoa mkono wa shukrani mara baada ya kupewa zawadi ya Mbuzi
wawili na wanakiji wa Mlowa Barabarani mara baada ya kuwasha umeme
katika hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa
Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard
Kalemani (katikati) akiwa na viongozi akikata utepe wa kuashiria
uzinduzi wa umeme katika hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa
kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard
Kalemani,akipiga makofi mara baada ya kuzindua uwashaji wa umeme
katika hospitali ya wilaya ya chamwino iliyojengwa kijiji cha Mlowa
Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard
Kalemani,akiwasha umeme katika hospitali ya wilaya ya chamwino
iliyojengwa kijiji cha Mlowa Barabarani iliyopo jijini Dodoma.
……………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nishati, Dk.Medard
Kalemani amesema hakuna kijiji cha jimbo la Mtera kitakachobaki kutokuwa
na umeme kufikia Juni mwaka 2020.
Aidha, ameagiza Shirika la Umeme nchini(Tanesco) kuhakikisha
linapeleka umeme katika vitongoji vyote vya Mlowa kuanzia wiki ijayo.
Kalemani ametoa kauli hiyo alipokuwa akiwasha umeme katika hospitali ya Mlowa wilaya ya Chamwino.
Amesema hadi Juni mwakani jimbo zima litakuwa na umeme kwenye
vijiji vyote na kazi ya kupeleka kwenye vitongoji itaendelea hadi Juni
2021.
“Leo tunapoongea kuna vijiji 38 ndani ya miaka minne na viwili
vinawaka umeme kesho vinafikia 40, naomba tumpongeze Rais John Magufuli
kwa kazi nzuri anayofanya,”amesema.
Ameeleza kuwa vijiji 20 vinavyobaki vipo kwenye mpango ambapo
vijiji vinne kati ya 20 vilivyobaki vitapelekewa umeme wiki ijayo na
Tanesco.
“Vijiji 16 vitakavyobaki vitapelekewa umeme mwezi februari 2020,”amesema.
Amewaonya Tanesco kutojaribu kuwatoza wananchi gharama kubwa ya kuunganisha umeme zaidi ya Sh.27,000.
“Msijaribu awe mkandarasi au Tanesco mwenyewe au REA
atakayefanya hivyo Meneja nikute umemfukuza, usipomfukuza nakufukuza
wewe,”amesema.
Kalemani amepiga marufuku ulipishaji wananchi nguzo za umeme na atakayetoza ajifukuzishe kazi mwenyewe.
Waziri huyo amesema kuwaka kwa umeme kwenye jimbo hilo kutaharakisha maendeleo.
“Rais ametoa fedha nyingi zaidi ya Sh.Bilioni 36 kuwaletea umeme
mkoa wa Dodoma, ni wajibu wenu kuchangamkia, nitakapokuja hapa tutakuja
kukagua,”amesema.
Kwa upande wake, Meneja Tanesco wilaya ya Chamwino Bw.Baltazar
Massawe,amesema umeme huo utasaidia wananchi kwenye shughuli mbalimbali
ikiwemo wanafunzi na walimu.
“Huduma za Afya zitaboreshwa kutokana na umeme kuwepo, wananchi wataweza kuanzisha viwanda vidogo vidogo,”amesema
Naye, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde amesema alimuomba Waziri huyo kufikisha umeme kwenye hospitali hiyo na akakubali.
“Kuna baadhi ya maeneo yamerukwa tunaomba umeme kwenye
vitongoji, nikuombe sana ujio wako uwe neema kwa kuhakikisha tunapata
umeme katika kitongoji cha Sokoine ambacho kuna mradi wa maji pale
lakini hakuna umeme,pia umeme ufike kwenye makanisa na
misikiti,”amesema.
0 comments:
Post a Comment