Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe akimkabidhi
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo ripoti
ya upotevu wa fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia leo
jijini Dar es Salaam
…………………..
Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeikabidhi TAKUKURU jalada la
kulifanyia uchunguzi upotevu wa fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini
Ethiopia
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe
amekabidhi jalada hilo kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia
Jenerali John Mbungo katika ofisi ndogo za Wizara jijiji Dar es Salaam.
Hatua hiyo imekuja kutokana na
jitihada za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John
Pombe Magufuli za kupambana na kuzuia rushwa pamoja na matumizi mabaya
ya fedha za uma.
Uchunguzi huo unafanyika baada ya kubainika upotevu/matumizi mabaya ya fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.
Kuhusu kiwango cha fedha
kilichopotea Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe, amesema kitajulikana mara baada
ya Takukuru kukamilisha uchunguzi huo wa jalada walililokabidhiwa.
0 comments:
Post a Comment