Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea mfano wa hundi ya gawio yenye
thamani ya Bilioni 11 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta
ya PUMA Energy Tanzania Dkt Selemani Majige (wa pili kushoto) akiwa
pamoja na Ofisa Mawasiliano na Mwanasheria wa Kampuni hiyo Goodluck
Shirima (kulia). Gawio hilo limekabidhiwa leo Ikulu Chamwino, Jijini
Dodoma. Katikati ni Spika wa Bunge, Job Ndugai na kushoto ni Waziri wa
Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango.
Godluck Shirima kutoka Kampuni ya
Mafuta ya Puma Tanzania(wa kwanza kushoto) akifuatilia hotuba ya Rais
Dk.John Magufuli wakati wa ghafla ya Taasisi, Mashirika na Kampuni
kukabidhi gawio kwa Serikali,ambapo Kampuni ya Puma amekabidhi gawio la
Sh.bilioni 11 kwa Rais Magufuli leo Novemba 24,Ikulu ya Chamwino jijini
Dodoma
Rais Dk.John Magufuli akiwa na
viongozi mbalimbali wa Taasisi,Mashirika na Kampuni baada ya tukio la
kukabidhiwa kwa gawio iliyofanyika leo Novemba 24,Ikulu ya Chamwino
jijini Dodoma
…………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAKURUGENZI wa Kampuni ya Puma
Energy Tanzania wamependekeza gawio la sh. bilioni 22 kwa mwaka
unaoishia Desemba mwaka jana ambapo kila mwanahisa atapata sh. bilioni
11.
Aidha, imesema kuwa mwaka 2017 gawio lilikuwa sh. bilioni 18, 2016 sh. bilioni 14 na mwaka 2015 sh. bilioni 9.
Mkurugenzi Mtendaji wa Puma
Energy, Dominic Dhanah aliitoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati
akikabidhi gawio la Sh.bilioni 11 kwa Rais Dk. John Magufuli Ikulu ya
Chamwino jijini Dodoma.
Amebainisha kuwa ni kuwa kampuni
inamilikiwa kwa pamoja na serikali (Kupitia Msajili wa Hazina, Wizara ya
Fedha) pamoja na Puma Investments Limited, kila moja ikiwa na umiliki
wa hisa kwa asilimia 50.
“Wakurugenzi wa kampuni
wamependekeza gawio la Sh.bilioni 22 bolioni kwa mwaka ulioishia Disemba
2018. Hivyo Kila mwanahisa atapata shilingi 11 bilioni. (2017 gawio
lilikuwa 18 bilioni, 2016 gawio lilikua 14 bilioni na 2015 gawio lilikua
9 bilioni.)
Amesema kuwa kutokana na utendaji
mzuri wa kampuni ya Puma Energy, gawio limekua kwa asilimia 57
ikilinganishwa na gawio la mwaka 2016 na kwa asilimia 22 ikilinganishwa
na gawio na mwaka 2017.
Amefafanua kuwa ukuaji huu
unaendana sambamba na mikakati ya kampuni ya kuhakiksha kampuni
inaendelea kukua, kutengeneza faida, kukuza ajira nchini, kuchangia pato
la taifa kupitia kodi, na kuendelea kuiunga serekali mkono katika
kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo,”imesema taarifa hiyo
Amesema kuwa kampuni ya Puma ni ya mkondo wa kati kimataifa
katika masula ya mafuta na pia kampuni ya mafuta inayojihusisha na
uhifadhi mkubwa na usambazaji.
Ameeleza kuwa majukumu makuu ya
kampuni ni masoko na usambazaji wa bidhaa za petroli ndani ya Tanzania.
Kampuni inauwezo wa kuhifadhi jumla ya lita za mafuta milioni 94, vituo
52 vya mafuta maeneo mbalimbali nchini na inahudumia viwanja vinane vya
ndege.
Amesema kuwa kufikia mwisho wa mwaka ulioishia Desemba 31
2018 kampuni ilitengeneza faida kabla ya kodi ya jumla ya Shilingi
bilioni 25 na iliwekeza takribani sh. bilioni 16 kwa mwaka 2018 kununua
na kuendeleza miundombinu ikiwemo ukamilishwaji wa mfumo wa kujazia
mafuta katika jengo namba Tatu (Termina 3) katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere Dar e salaam.
Aidha, ununuzi wa vituo viwili vya mafuta kwenye jiji la Dodoma ikiwa ni kuiunga serekali mkono katika kuhamia Dodoma.
Aliweka wazi kuwa ufanisi wa
kibiashara wa Puma kwa mwaka 2018 ulikua mzuri kwa pande zote za mauzo
pamoja na mapato na unatokana na biashara ya mafuta ya ndege ambako kwa
sasa sisi ndio tunaongoza katika soko.
Pia, amesema kuwa taaarifa za
masoko zilizochapishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji(EWURA)
inaonesha kuwa uwepo wa Puma Energy kwenye soko la mafuta umeongezeka
kutoka asilimia 12 mwaka 2015 hadi asilimia 14 kwa mwaka 2017.
Ameongeza kuwa juhudi za serikali
ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli na Serikali yake katika
mikakati yake ya kukusanya kodi, kutoa fursa kwa wawekezaji wa nje na
ndani na kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati kama ilivyooneshwa kwenye
bajeti ya 2019/20.
Amesema kuwa mikakati hiyo imewezesha kampuni hiyo kupata
kazi ya kuuza mafuta katika mradi wa reli ya kati “standa gauge”, mradi
wa bwawa la umeme la Mwl. Julias Nyerere kule Rufiji, Daraja jipya la
Salender na miradi mingine mingi ya kimkakati.
Amefafanua kuwa miradi hiyo
mikubwa inatoa fursa kwa wawekezaji mbali mbali kufanya biashara na
kufanya makampuni mengi ikiwemo Puma kutengeneza faida zaidi.
Ameongeza kuwa, Puma itaendelea
kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Serikali ya Awamu ya tano, na
kuendelea kuchangia katika maendeleo ya taifa, hivyo uongozi wa
utaendelea kutoa ushrikiano kama ambavyo wamekua wakishirikiana siku
zote.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya
Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy, Dk. Selemani Majige amesema kuwa
gawio la sh. bilioni 11 walilotoa linaweza kuwa ni dogo lakini kwa sasa
wanapambana kuhakikisha linaongezeka.
“Lazima tuonyeshe kuwa Puma ni
kampuni ya mafuta inayoongoza kwa biashara nchini, tuna vituo maeneo
mbalimbali hivyo watanzania watuunge mkono kwenye ununuzi wa mafuta ili
kuleta maendeleo,”amesisitiza Dkt.Majige
0 comments:
Post a Comment