Waziri wa Katiba na Sheria wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi, Dkt.Augustine Mahiga akiongoza
Mkutano wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa nchi za Asia na
Afrika(AALCO) Uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam, Katika Mkutano huo Waziri Mahiga
alikabidhiwa kuwa Rais wa AALCO
Katibu Mkuu kutoka Wazira ya
Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome akizunguma na wageni wa Mkutano wa
Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa nchi za Asia na Afrika(AALCO)
kuhusu kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko tanzania bara na Zanzibar
mara baada ya kumaliza Mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Shirika la
Mashauriano ya Kisheria kwa nchi za Asia na Afrika(AALCO), Prof. Kennedy
Gastorn akiteta jambo na Mjumbe kutoka Sekritarieti ya AALCO mara baada
ya kumaliza Mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Katiba na Sheria wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi, Dkt.Augustine Mahiga,
akisalimia na Mmoja wa Washiriki wa Mkutano wa AALCO mara baada ya
kumaliza Mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Katiba na Sheria wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi, Dkt.Augustine Mahiga,
akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria
kwa nchi za Asia na Afrika(AALCO), Prof. Kennedy Gastorn na Mkurugenzi
Mkuu wa Sheria za Kimataifa kutoka Nigeria, Mhe.Wilfred Ikatari
Waziri wa Katiba na Sheria wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi, Dkt.Augustine Mahiga, akiwa
kwenye picha ya pamoja na Washiriki wa Mkutano wa AALCO mara baada ya
kumaliza Mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam
…………………….
Na. Paschal Dotto-MAELEZO
Shirika la Mashauriano ya Kisheria
kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambalo kikao chake cha 58
kimemalizika hapa Jijini Dar es Salaam safari hii kimeteua Tanzania kuwa
Rais wa Shirika hilo na kwa maana hiyo Waziri wa Katiba na Sheria
Tanzania, Balozi Augustine Mahiga anashika nafasi hiyo.
Kikao hicho kilichoanza
jumatatu, wiki hii kimemalizika leo naajenda mbalimbali zilijadiliwa
huku msukumo ukilenga kuimarisha sheria za ukanda wao na Kimataifa kwa
Ujumla.
Akizungumza na waandishi wa
habari Waziri wa Katiba na Sheria kutoka Tanzania ambaye ameanza wadhifa
wake Rais Mpya wa AALCO amesema kuwa katika mfululizo wa vikao vyao
kitu kikubwa kilichojadiliwa ni suala la vikwazo dhidi ya mataifa
ambalo limekuwa tatizo kwa nchi mbalimbali.
“Mkutano huu ulikuwa
unaangazia masuala mbalimbali na muhimu kwa nchi za Afrika na Asia na
kwingineko duniani na suala ambalo lililpewa kipaumbele ni kuhusu
vikwazo ambavyo nchi mbalimbali kubwa duniani zimekuwa zikiziwekea nchi
ndogo, kitu ambacho kinaumiza wananchi katika nchi hizo”, amesema,
Balozio Mahiga.
Balozi Mahiga, amesema kuwa
Mkutano huo ambao washiriki wake ni kutoka Asia na Afrika unazingatia
masuala mengi ya kisheria, likiwemo lile la vikwazo kwa nchi kama za
Zimbabwe, Palestine, Iran na nyinginezo duniani.
Alieza kuwa suala la kuweka
vikwazo halijadiliwi na nchi moja , wala mbili au tatu ambazo ni kubwa
na kuwa zinajiweza kiuchumi, bali suala hilo ni la Chombo cha Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa, na hufikiwa ikiwa kuna wasiwasi wa
kiusalama kwa nchi moja hiyo inayowekewa vikwazo, kwa hiyo suala la
vikwazo lilikuwa kipaumbele kwenye mkutano wa AALCO.
Aidha Mkutano huo wa 58 wa
AALCO ulijadilii mambo mengine sita, likiwemo lile la matumizi na
utajiri ulioko baharini, rasilimali kama vile mafuta, madini na samaki
ambavyo vinahitajika sana duniani, “kwa hiyo lilikuwa ni jambo jema
kujadili vitu hivyo muhimu kwa nchi za Afrika na Asia.” Amesema Rais wa
AALCO.
“katika Mkutano huu wa AALCO
tumezungumza na kubadilishana mawazo kuhusu utajiri ulioko kwenye
bahari, ambapo kila mmoja anautaka, hivyo tunatakiwa tuweke sheria nzuri
na vyombo vya kisheria ambavyo vitatufanya kutumia vitu hivyo bila
kugongana sehemu” Balozi Mahiga.
Aliongeza kuwa katika masuala
saba yaliyojadiliwa, suala la vikwazo na matumizi ya bahari ni busara
kuyajadili hayo katika majukwaa mbalimbali ikiwemo AALCO; ili kuiambia
dunia kuhusu kukua kwa maendeleo ya Sheria za Kimataifa.
Tanzania itakuwa Rais wa AALCO
kwa muda wa mwaka mmoja, ambapo Mkutano wa 59 unaotarajiwa kufanyika
Bara la Asia, Nchini China, ambapo Tanzania itakabidhi kiti hicho kwa
China.
0 comments:
Post a Comment