![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/1-75.jpg)
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwasha mshumaa katika kaburi
la Baba wa Taifa Mawalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa Maadhimisho
ya Miaka 20 ya kifo chake katika kijiji cha Mwitongo Butiama mkoa wa
Mara leo tarehe 14 Oktoba 2019.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/2-62.jpg)
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Wa pili kushoto) pamoja na
viongozi wengine wakiwa mbele ya kaburi la hayati Baba wa Taifa Mwalimu
Nyerere Maadhimisho ya Miaka 20 ya kifo chake katika kijiji cha Mwitongo
Butiama mkoa wa Mara leo tarehe 14 Oktoba 2019. Kulia ni Waziri Mkuu
Mstaafu Joseph Sinde Warioba na wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi Phillip Mangula.![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/deb92d62-2686-4a6f-8b5a-5683c7d6e7f9.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/deb92d62-2686-4a6f-8b5a-5683c7d6e7f9.jpg)
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Wa tatu kulia) pamoja na
viongozi wengine wakiwa nje ya Kanisa Katoliki Parokia ya Butiama mara
baada ya Misa ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika
Maadhimisho ya Miaka 20 ya kifo chake katika kijiji cha Mwitongo Butiama
mkoa wa Mara leo tarehe 14 Oktoba 2019. Wa kwanza kushoto ni Waziri
Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba na wa pili kushoto ni Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Phillip Mangula. Kulia ni Mbunge wa
Jimbo la Musoma Vijijini Sospeter Muhongo na wa pili kushoto ni Mkuu wa
Mkoa wa Mara Adam Malima.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).
********************************
Na Munir Shemweta, WANMM BUTIAMA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula amewataka vijana kujifunza maisha ya baba
wa Taifa Mwalimu Julius kwa vitendo ili matendo ya kiongozi huyo wa
kwanza wa Tanzania yaendelee kukumbukwa.
Akiwa katika Maadhimisho ya miaka
20 ya kumbukumbu ya Mwl. Nyerere katika kanisa Katoliki la Bikira Maria
jimbo la Musoma Parokia ya Butiama mkoani Mara leo tarehe 14 Oktoba 2019 Dkt
Mabula alisema, ni vyema vijana wa watanzania wakatumia hazina ya wazee
kama Mwl Nyerere Julius Nyerere kuwa chachu ya kuishi kwa vitendo.
“Niwaombe vijana kutumia hazina ya wazee wetu na kuwa chachu ya kuishi kwa vitendo” alisema Dkt Mabula.
Dkt Mabula ambaye alikuwa Mkuu wa
kwanza wa wilaya ya Butiama mkoani Mara alihitimisha salamu zake za
miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere wilayani Butiama kwa kuwataka
wananchi kuishi pia kwa kumcha Mungu kwa kuwa wakati wa uhai wake baba
wa taifa aliishi kwa kumcha Mungu.
Kwa upande wake Waziri Mkuu
Mstaafu Joseph Sinde Warioba alimueleza Mwl Nyerere kuwa alikuwa ni mtu
wa maisha ya Mungu aliyejitahidi kujenga umoja na mshikamano kwa nchi
yake na Bara la Afrika kwa ujumla.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama
cha Mapinduzi (CCM) Phillip Mangula alimuelezea Mwl Nyerere kama mtu
aliyepigania haki na aliyesisitiza kuwa binadamu wote ni ndugu na Afrika
ni moja.
Maadhimisho ya miaka 20 ya
kumbukumbu ya Mwl Nyerere katika kanisa katoliki Parokia ya Butiama
mkoani Mara yalihudhuriwa pia na Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima,
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Steven Wasira, Mbunge wa Jimbo la Musoma
Vijijini Sospeter Muhongo, Chief Wanzagi, Mkurugenzi wa Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC) Dkt Maulid Banyani na Mkurugenzi wa Shirika la
Reli Tanzania Masanja Kadogosa.
0 comments:
Post a Comment