
*****************************
RAIS wa Urusi, Vladimir Putin amefungua Kongamano la Biashara
baina ya Urusi na Afrika (Russia Business Forum) ambapo amesema Bara la
Afrika ni muhimu katika maendeleo ya uchumi wa dunia na ni kivutio
kikubwa kwa wafanyabiashara wa Urusi.
Ameyasema
hayo leo (Jumatano, Oktoba 23, 2019) wakati akihutubia mkutano huo
uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Olympic Park katika mji wa Sochi
nchini Urusi. Rais Putin amesema takwimu zilizotolewa na watalaamu wa
masuala ya uchumi zinaonyesha kwamba pato la Afrika (GDP) litafikia dola
trilioni 29 ifikapo 2050.
Amesema
biashara kati ya Urusi na Afrika imeongezeka mara dufu katika kipindi
cha miaka mitano iliyopita na kufikia dola za Marekani bilioni 20 na
kwamba nchi yake inaunga mkono wazo la kuanzishwa eneo huru la biashara
katika bara la Afrika ukiwa ni mkakati wa Umoja wa Afrika (AU) na kwamba
itatoa ushirikiano ili kufanikisha wazo hilo.
Kadhalika,
Rais Putin ameongeza kuwa nchi yake inatekeleza kwa vitendo mpango
kuzifutia madeni nchi za Afrika na hadi sasa imeshafuta madeni ya zaidi
ya dola za Marekani bilioni 20.
Amesema
utoaji wa mafunzo ya taaluma mbalimbali umekuwa ni utamaduni wa
ushirikiano kati ya Urusi na Afrika. “Hadi katikati ya miaka ya 80 nchi
yake imejenga taasisi zipatazo 100 za mafunzo mbalimbali Barani Afrika
na watu 500,000 wampata mafunzo katika taasisi hizo.
Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa ameshiriki katika mkutano huo akimwakilisha Rais John
Pombe Magufuli. Pamoja naye idadi kubwa ya Wakuu wa Nchi na Serikali
katika Bara la Afrika wamehudhuria mkutano huo.
Miongozi mwa
viongozi hao ni Rais Yoweli Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa
Rwanda, Rais wa Misri na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Abdel Fattah al
Sissi, Rais wa Afrika ya Kusini, Cyril Ramaphosa, Rais wa Zimbabwe,
Emmerson Mnangagwa, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi na viongozi wengine
kutoka Bara la Afrika.
Kesho
(Alhamisi, Oktobba 24, 2019) Waziri Mkuu anatarajia kushiriki katika
mkutano baina ya Urusi na Wakuu wa nchi na Serikali wa Bara la Afrika.
0 comments:
Post a Comment