Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akiwasha umeme
katika moja ya nyumba za Mkazi wa Kijiji cha Muheza katika Halmashauri
ya Mji wa Kibaha ikiwa ni kuzindua Mradi wa Usambazaji wa Umeme katika
vijiji vilivyopo pembezoni mwa Miji( Peri-Urban) katika wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu(kushoto) akiteta jambo na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA),
Wakili Julias Bundala Kalolo( kulia) kabla ya kuwasha umeme na kuzindua
Mradi wa Kusambaza umeme katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa Miji (
Peri-Urban) katika Halmashauri ya Kibaha vijijini mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akikata utepe
kuashiria kuzindua Mradi wa Usambazaji wa Umeme katika vijiji vilivyopo
pembezoni mwa miji( Peri-Urban) katika Kijiji cha Mwanabwito wilayani
Kibaha vijijini.Uzinduzi huo umeshuhudiwa na Wajumbe bodi ya Wakurugenzi
ya REA ,Viongozi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake
ikiwemo REA na Tanesco.
Wasanii wa nyimbo za asili kutoka kabila asili ya Mkoa wa
Pwani,wakiigiza kumtambikia Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu( kulia
aliyekaa) wakati wa sherehe za kuzindua Mradi wa Usambazaji wa Umeme
katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa miji( Peri-Urban) wilayani Kibaha,
mkoani Pwani.
Gari lililobeba nguzo mali ya Mkandarasi Sengerema zikiwa tayari
zimewasili katika kijiji cha Mwanabwito, katika Halmashauri ya Kibaha
vijijini kwa ajili ya mradi wa Peri-Urban.
……………………………………………………………..
Na Zuena Msuya, Pwani
Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu, amesema zaidi ya wateja 6000
mkoani Pwani wataunganishiwa umeme wa mradi wa kusambaza umeme katika
vijiji vilivyopo pembezoni mwa Miji.
Mgalu alisema hayo, Augosti 05,2019, wakati akiwasha na kuzindua
umeme katika kijiji cha Muheza katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha na
katika kijiji cha Mwanambwito katika Halmashauri ya Kibaha vijijini.
Alisema kuwa maeneo yote ya Wilaya ya Kibaha ikiwemo mitaa, vijiji pamoja na vitongoji vyate vitafikiwa na Mradi wa Peri-Urban.
Alifafanua kuwa mradi huo utangarimu zaidi ya shilingi bilioni 14
katika Mkoa wa Pwani pekee na unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha
miezi 9 baada ya kuanza kwa utekelezaji wake.
Aliweka wazi kuwa mradi huo utaleta tija kubwa kwa taifa kwa kuwa
utakuwa ukifanya kazi ya kuwaungashia umeme wananchi ambao hawakupitiwa
na Mradi wa kusambaza umeme vijijini( REA) au hawakuweza kupata huduma
hiyo kutokana na sababu mbalimbali.
“Mradi huu utafanya kazi kubwa sana kwa wananchi na utaleta manufaa
makubwa sana kwa sababu wale wote walioshindwa kuunganishwa na umeme wa
REA kwa namna moja au nyingine, au wale ambao hawakupitiwa kabisa, sasa
mradi huu unamaliza kila kitu, utawaunganisha wote,jiandaeni
kuupokea”,alisisitiza Mgalu.
Aliwaeleza wananchi wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani kuwa
wataunganishwa na mradi huo kwa bei ya shilingi 27,000/= tu,ambayo
inajumuisha gharama za nguzo, nyaya pamoja na LUKU, hivyo wananchi
wasikubali kuchangia zaidi ya kiasi hicho cha fedha.
Sambasamba na hilo aliwaeleza kuwa mwananchi atalipia gharama ya
kutandaza nyaya katika nyumba yake,kwa makubaliano na wakandarasi au
mafundi waliothinishwa na shirika la Umeme nchini (TANESCO), kufanya
shughuli hizo.
Mradi huu kwa Mkoa wa Pwani unatekelezwa na mkandarasi mzawa wa
kampuni ya Sengerema na tayari ameanza kutekeleza mradi huo kwa
kuwaungaishia wananchi huduma ya umeme huku akiendelea na ujenzi wa
miundombinu katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Pwani.

0 comments:
Post a Comment