METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, August 3, 2019

ZAIDI YA BILIONI SITA ZATUMIKA KULETA MAENDELEO KATA YA MAPANDA

Diwani wa kata Mapanda Obadia Kalenge akielezea jinsi gani walivyotumia mabilioni ya fedha kwa ajili ya kuleta maendeleo katika sekta ya elimu,miundombinu,afya na utamaduni
 
NA FREDY MGUNDA, IRINGA.
 
Zaidi ya bilioni sita
zimetumika kuleta maendeleo katika sekta ya elimu,miundombinu,afya na utamaduni
katika kata ya Mapanda iliyopo katika jimbo la Mufindi kaskazini ikiwa ni
kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 hadi 2020.
 
Akizungumza diwani
wa kata hiyo Obadia Kalenge alisema kuwa katika sekta ya elimu wamefanikiwa
kujenga majengo mapya katika shule mbalimbali zilizopo katika kata hiyo kwaushirkiano
wa serikali,wananchi na wadau mablimbali wa maendeleo waliopo katika kata hiyo.
 
“Nguvu ya wananchi ilikuwa ni
mchanga na mawe tu,mfano shule ya Kihansi pekee yake ina miradi inayogharimu
kiasi cha shilingi milioni mia sita themanini na nane na laki tano hivyo nina
shule saba na jumla ya shilingi milioni mia nane na sitini zimetumika kuleta
maendeleo kwenye elimu katika kata yangu ya Mapanda” alisema Kalenge
 
Kalenge alisema kuwa katika
sekta ya afya amefanikisha uwepo wa CTC kuwepo kwenye kata hiyo na kuanza
kujenga jingo la wodi ya akina mama na watoto na kuendelea na ujenzi wa kituo
cha afya na kata ya hiyo inavijiji vitano hivyo kila kijiji kina zahanati
ambayo imekuwa ikasidia kuta huduma ya afya kwa wananchi wa kata hiyo.
 
“Mwaka jana wakati wa bajeti
nilijenga hoja kwenye baraza la madiwani kwa kuomba kujengewa kituo cha afya
ambapo halmashauri walinikubaria ombi langu na kuhakikisha mwisho mwa 2019
kituo hicho cha afya kinakuwa kimeanza kufanya kazi” alisema Kalenge
 
Kila zahanati kuna mganga na
nesi  na kuongeza kila zahanati zilizopo
katika kata hiyo kuna pikipiki ambazo zimekuwa zikisaidia katika usafiri  wa hapa na pale kutokana na mazingira ya kata
hiyo hivyo usafiri wa pikpiki umekuwa ukirahisisha utendaji kazi kwa watumishi
wa afya wa kata hiyo.
 
Aidha Kalenge alisema kuwa
swala la barabara limekuwa changamoto kubwa kutokana na barabara hizo
kuharibika mara kwa mara na zinatumia gharama kubwa kukarabati miundombinu hiyo
laki kuna barabara ya kutoka Chogo hadi Isipi kwa mara ya kwanza ndio
imetengenezwa kwa mara ya kwanza toka kuumbwa kwa dunia.
 
“Ili kurahisisha maendeleo
lazima kuwe na miundombinu bora hivyo nimepigana navyoweza kwa ushirikiano
mkubwa na mbunge wa jimbola Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa tumefanikiwa
kutatua kero hiyo kwa kiasi chake” alisema Kalenge
 
Kalenge alisema kuwa tatizo la
maji linaelekea kutatuliwa kutokana najuhudi zinazofanywa kuhakikisha wananchi
wa kata hiyo wanapata maji kwa kutumia mamilioni ya fedha kutoka kwa wadau na
serekali ambapo wananchi wameshachanga na serikali tayari imeleta wataalamu kwa
ajili ya kutatua kero hiyo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com