METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, August 15, 2019

MBUNGE MGIMWA AKERWA NA UBOVU WA BARABARA ZA KATA YA MAPANDA

 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kitongoji cha Mtwivila kilichopo kijiji cha Mapanda kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara
 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kitongoji cha Mtwivila kilichopo kijiji cha Mapanda kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara
 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa  kijiji cha Chogo kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kijiji cha Ihimbo kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara
 
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
Wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini
wanakabiliwa na changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara ambayo imekuwa
ikirudisha nyuma maendeleo kutokana na wananchi kutofanya kazi kwa uhuru.
 
Akizungumza wakati wa ziara
yake kwenye kata ya Mapanda Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa

amekiwa kuwa tatizo la ubovu wa miundombinu hiyo imekuwa kero na ameanza
kuifanyia kazi ili kuzikarabati ziweze kupitika kirahisi.
 
“Nimebaini kuwepo kwa uchakavu
wa barabara katika kata ya Mapanda ambazo zimekuwa zikififisha maendeleo ya
jimbo langu hivyo natakiwa kufanya kila niwezalo kuhakikisha barabara hizi
zinapitika” alisema Mgimwa
 
Mgimwa amesema
kuwa amefaikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutengeza barabara zote
korofi ili ziweze kupitika kwa urahisi.
 
“Nimefakisha kupata zaidi ya
shilingi milioni mia nane kuhakikisha tunakarabati barabara hii ambayo imekuwa
inatumiwa na watu wengi kimaendeleo katika jimbo hili” alisema Mgimwa
 
Mgimwaalisema kuwa kuna
barabara inayotoka kuanzia Kibengu,Kipanga,Ihimbo,Uhafiwa,Kisusa,Ukami hadi
njia panda ya Mapanda inayokadiliwa kuwa na urefu wa kilometa sitini na moja
imetengewa fedha kidogo tofauti na matengenezo yanayotakiwa kufanyika katika
barabara hiyo.
 
“Nitakuja na viongozi wa TARURA
huku kuhakikisha wanajionea ubo vu wa barabara hizi ili wanavyotenga fedha
wajue wanakarabati wapi na wanaacha wapi haiwezekani barabara hii ikatengewa
kiasi cha shilingi milioni thelethini tu” alisema Mgimwa
 
Aidha Mgimwa amewataka
TANROAD na TARURA kuzikarabati  barabara
zote korofi kipindi cha kiangazi  ili
zipitike kirahisi na sio kipindi cha masika ambapo mara nyingi hutokea kero kwa
wananchi.
 
Wakitoa kilio chao kwa mbunge huyo
wanachi wa vijiji hivyo walimwambia hakuna maendeleo yanayoendelea katika
vijiji hivyo kutokana na ubovu wa barabara hizo.
 
Hakuna usafiri wa basi wala gari
inayofika huku kutokana na ubovu wa barabara hizi hivyo tunakuomba uhakikishe
unatusaidia kuzikarabati barabara hizo” walisema wananchi 
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com