
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu
akizungumza na wafanyakazi wa Shamba la Katani la Hassan Sisal Estate
lililopo Makanya, Wilayani Same alipotembelea shamba hilo kufuatia
maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu masuala ya kazi
aliyoyatoa Julai 20, 2019 alifanyaziara Mkoani Kilimanjaro.

Meneja Mshauri wa Shamba la Katani
la Hassan Sisal Estate, Bw. Ndekirwa Nnyari (Kushoto) akitoa maelezo
kuhusu shamba hilo na masuala ya wafanyakazi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama alipofanya ziara katika shamba hilo Julai 27, 2019.

Baadhi ya wafanyakazi wa Shamba la
Katani la Hassan Sisal Estate wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipofanya ziara katika shamba hilo
kufuatia maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu masuala ya
kazi aliyoyatoa Julai 20, 2019 alifanyaziara Mkoani Kilimanjaro.

Sehemu ya Wataalamu walioambana na
Mhe. Waziri na wafanyakazi wa Shamba la Katani la Hassan Sisal Estate
wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani)
alipofanya ziara katika shamba hilo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama akiteta jambo na Afisa Kazi Mfawidhi kutoka Mkoa wa Kilimanjaro
Bw. Mwinyi Mkuu wakati wa ziara yake Wilayani Same katika Shamba la
katani la Hassan Sisal Estate.

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Large Mature akifafanua jambo kuhusu
uwasilishaji wa michango ya wafanyakazi wa Shamba la katani la Hassan
Sisal Estate.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama akihakiki malipo ya wafanyakazi wa Shamba la katani la Hassan
Sisal Estate alipokuwa akioneshwa na Meneja Mkuu wa Unique Consultance
Bw. Edwin David (Kulia) . Afisa Kazi Mfawidhi kutoka Mkoa wa Kilimanjaro
Bw. Mwinyi Mkuu (katikati).

Mmoja wa Wafanyakazi wa Shamba la
katani la Hassan Sisal Estate Bw. Salum Issa akimwelezea Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani), changamoto wanazokumbana
nazo katika utendaji kazi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama akisikiliza kero kutoka kwa mfanyakazi wa Shamba la katani la
Hassan Sisal Estate, alipofanya ziara kwenye shamba hilo Julai 26, 2019
kwa lengo la kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa
kuhusu masuala ya kazi aliyoyatoa Julai 20, 2019.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemery Staki
(kulia), alipofanya ziara Wilayani huo kwa lengo la kufuatia maagizo ya
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu masuala ya kazi aliyoyatoa
Julai 20, 2019.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama na Meneja Mshauri wa Shamba la Katani la Hassan Sisal Estate,
Bw. Ndekirwa Nnyari (katikati) akiwatambulisha baadhi ya viongozi wa
Shamba la katani la Hassan Sisal Estate.
***************
Na; Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama ametoa maagizo kwa viongozi wa Shamba la Katani la
Hassan Sisal Estate kuhakikisha wanatatua migogoro na wafanyakazi pamoja
na kusimamia haki zao ipasavyo.
Waziri Mhagama ametoa maagizo hayo
wakati wa ziara yake Wilayani Same alipofanya ziara katika Shamba la
Hassan Sisal Estate ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe.
Kassim Majaliwa kuhusu masuala ya kazi aliyoyatoa Julai 20, 2019
alipotembelea shamba hilo lililopo Mkoani Kilimanjaro, Wilaya ya Same.
Akizungumza na wafanyakazi pamoja
na viongozi wa shamba hilo, alieleza kuwa waajiri wanatakiwa kutekeleza
matakwa yote ya Sheria za ajira na mahusiano kazini kwa kuzingatia
miongozo na kanuni ambayo inasimamia haki za msingi kwa wafanyakazi.
“Tunataka kuona ninyi kama waajiri
mnakuwa na vikao vyenye tija na wafanyakazi katika kuleta suluhu ya
masuala mbalimbali ya kazi,” alisema Mhagama
Aliongeza kuwa Kampuni mbili
zilizopo katika shamba hilo yaani Unique Consultancy na UPAMI
kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wafanyakazi hao, ikiwemo kuwasilisha
michango kwa wakati kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Pamoja na hayo alishauri pia
kampuni hizo kuwaweka wazi wafanyakazi kuhusu mikataba yao.
“Malalamiko na Manung’uniko ya
wafanyakazi ni mengi, mnatakiwa kukaa na kujadili pamoja namna bora ya
kutatua matatizo yao yanayojitokeza hususani kwenye mikataba,” alisema
Mhagama.
Katika hatua hiyo, Mhe. Mhagama
alimuagiza Meneja wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA),
kufanya kanguzi za mara kwa mara katika shamba hilo na kuangalia kama
wafanyakazi wanakabidhiwa vifaa vya kujinginga na madhara kazini
(Protective gears) kwa wakati, pamoja na kusimamia zoezi la upimaji afya
kwa wafanyakazi hao.
Pia, alitoa maelekezo kwa Meneja
wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Kilimanjaro,
kukabidhi kadi za uwanachama kwa wafanyakazi wa shamba hilo la Hassan
Sisal Estate na kufuatilia uwasilishaji wa michango yao kutoka kwa
waajiri wao.
Sambamba na hilo, Waziri Mhagama
ametaka Afisa Kazi Mfawidhi wa Mkoa wa Kilimanjaro kutembelea shamba
hilo na maeneo mengine mbalimbali katika mkoa huo ili kuelimisha
wafanyakazi sheria mbalimbali za kazi na ajira zitakazo wawezesha
kutambua haki zao za msingi.
Aidha, Waziri Mhagama alitoa
maelekezo juu ya uwepo wa vyama vya wafanyakazi kwenye mashamba yote ya
katani yaliyopo nchini, vitakavyosadia kuongeza tija na ufanisi katika
shughuli mbalimbali za utendaji kazi.
Pamoja na hayo, Mheshimiwa Mhagama
aliwataka viongozi wa shamba hilo kuendelea kusimamia vizuri maslahi ya
wafanyakazi wao ili waweze kutekeleza majukumu ya kila siku wanapokuwa
katika maeneo yao ya kazi.
Naye, Meneja Mshauri wa Shamba
hilo, Bw. Ndekirwa Nnyari aliahidi kufanyia kazi maagizo yote
yaliyotolewa ikiwemo kuwa na majadiliano ya mara kwa mara na wafanyakazi
kwa itakayowapa munufaa ya pamoja.
Kwa upande wake, Meneja wa Mfuko
wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Victor Luvena amesema kuwa
watatekeleza maagizo yaliyotolewa na Mheshimiwa Waziri kwa kuchukua
hatua za kisheria kwa wale watakaoshindwa kutekeleza.
Pia mmoja wa Wafanyakazi wa Shamba
hilo, Bi. Cheshi Juma alisema kuwa ujio wa Waziri na wataalamu
alioambatana nao utasaidia kuondoa kero za wafanyakazi na kujenga
mahusiano mazuri na waajiri wao.
“Tumehamasika sana kuona Serikali
yetu ipo pamoja nasi katika kutetea maslahi ya wafanyakazi na
kushughulikia kero tulizokuwa tukikabiliana nazo katika maeneo ya kazi,”
alisema Cheshi
0 comments:
Post a Comment