Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM)
wilayani Bahi,Bw.Kadoke Hassan,akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati akitoa mikakati ya chama kuelekea katika
uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Mchungaji wa Kanisa la Uamsho Pentecoste,Damian Mchela,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Aliyekuwa mwanachama wa Chadema wilaya ya
Bahi,na Mgombea wa Ubunge ,na sasa ni kada wa CCM Bw.Mathias
Lyamunda,akitoa tathmini ya chama chake cha CCM kuelekea Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa.
………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi
[UVCCM]Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma umesema kuwa chama hicho kitashinda
kwa kishindo kwa asilimia mia moja [100%] kwenye mitaa yote ya wilaya
hiyo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa .
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Bahi Bw.Kadoke Hassan wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Wilayani humo.
Bw.Kadoke amebainisha misingi madhubuti
itakayokipaisha chama hicho ni kutokana na Uongozi mzuri na Maridadi
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta.John Pombe Magufuli
ikiwa ni pamoja na ununuzi wa ndege,mradi wa bomba la kusafirishia
Mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania,pamoja Mradi wa
reli ya kisasa .
Bw.Kadoke amehamasisha vijana wote
kushikamana na kujitokeza katika ushiriki wa serikali za mitaa na
wasisite kuyatangaza Mazuri yanayofanywa na Rais Magufuli.
Aidha ,UVCCM wilaya ya Bahi umechukua
fursa ya kumpongeza Mathias Lyamunda aliyekuwa Upinzani CHADEMA na
alishawahi kugombea nafasi ya ubunge na sasa kuhamia chama tawala cha
CCM Pamoja na wanachama wengine waliojiunga na chama hicho.
Katika hatua nyingine Bw.Kadoke amezungumzia juu ya baadhi ya viongozi wa dini kuacha kuchanganya na Masuala ya siasa .
Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la
Uamsho Pentecoste Bahi ,Damian Mchela amesema wao kama viongozi wa
dini wataendelea kuhubiri amani na kutii mamlaka ya serikali.
“Sisi kama viongozi wa dini hubiri kubwa
kwetu ni amani na kutii mamlaka ya serikali hivyo,tunaipongeza sana
serikali ya awamu ya tano kwa kuendelea kupambana na rushwa,pamoja na
kusaidia wanyonge na watanzania wa hali ya chini”
0 comments:
Post a Comment