MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia
Nyamoga,ambaye alikuwa mgeni rasmi katika fainali ya Buchimwe Cup 2019
akisalimiana na wachezaji wa timu zote mbili za Buigiri Mission na
Songambele kabla ya fainali ambapo Buigiri Mission waliibuka mabingwa
wapya kwa kuwachapa magoli 4-1 Songambele kwa mkwaju wa Penalti.
Wachezaji wa timu ya Songambele
wakisalimiana na wachezaji wa Buigiri Mission kabla ya Fainali ya
Buchimwe Cup 2019 ambapo Buigiri waliibuka mabingwa kwa kuwachapa
Penalti 4-1.
Wamuzi wakiwa na manahodha wa timu za
Buigiri Mission na Songambele katika fainali ya Buchimwe Cup 2019 ambapo
Buigiri Mission waliibuka mabingwa kwa kuwachapa 4-1 kwa njia ya
Penalti.
MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia
Nyamoga,akifurahi jambo na Diwani wa kata ya Buigiri Mhe.Kenneth Yindi
ambaye aliandaa mashindano ya Buchimwe Cup 2019 alipowasili kushuhudia
Fainali baina ya Buigiri Mission na Songambele.
MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia
Nyamoga,akisalimiana na baadhi ya viongozi waliohudhuria fainali ya
Buchimwe Cup 2019 iliyoandaliwa na Diwani wa kata ya Buigiri Mhe.Kenneth
Yindi.
MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia
Nyamoga,(katikati) akishuhudia Fainali ya Buchimwe Cup 2019 kati ya
Buigiri Mission na Songambele ambapo Buigiri waliibuka mabingwa wapya
kwa kuichapa magoli 4-1 Songambele kwa mikwaju ya Penalti akiwa na
Diwani wa kata ya Buigiri kulia Mhe.Yindi ambaye ndo muandaaji wa
michuano hiyo.
MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia
Nyamoga,akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Buchimwe
Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa kata ya Buigiri Mhe.Kenneth Yindi
wa kwanza kulia ambapo timu ya Buigiri Mission waliibuka mabingwa wapya
wa michuano hiyo kwa kuichapa 4-1 Songambele kwa Mikwaju ya
Penalti,shujaa akiwa golikipa wa Buigiri akipangua mashuti matatu ya
Songambele.
MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia
Nyamoga,akitoa zawadi kwa baadhi ya wachezaji walioibuka wachezaji bora
wa Mashindano hayo ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa kata
ya Buigiri Mhe.Kenneth Yindi ambapo timu ya Buigiri Mission iliibuka
kuwa bingwa kwa kuichapa magoli 4-1 Songambele kwa mikwaju ya Penalti.
MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia
Nyamoga,akimkabidhi Kombe Nahodha wa Buigiri Mission baada ya kuibuka
Mabingwa wapya wa Buchimwe Cup kwa kuichapa magoli 4-1 Songambele katika
Fainali hiyo.
Wachezaji wa Buigiri Mission Mabingwa
wapya wa Buchimwe Cup 2019 wakishangilia na Kombe lao baada ya kuichapa
magoli 4-1 Songambele kwa Mikwaju ya Penalti.
…………………………
Na.Alex Mathias,Chamwino
MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia
Nyamoga amesema kuna haja ya walimu wa timu za Taifa kuangalia vipaji
ambavyo vinapatikana maeneo ya vijijini.
Hayo ameyatoa wakati akifunga mashindano
ya Buchimwe Cup 2019 yaliyofanyika katika uwanja wa Shule ya Sekondari
Buigiri ambapo mchezo wa fainali ulizikutanisha timu za Buigiri Mission
na Songambele.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema vijijini
kumekuwa na vipaji vya hali ya juu lakini anakosekana mtu wa kuwashika
mkono hivyo akawaomba walimu wa timu za Taifa kufika katika maeneo hayo.
“Waje na hapa kwetu Chamwino kuna vipaji
vya hali ya juu naamini hata wale Algeria waliochukua AFCON kupitia
vipaji hivi ninavyoviona hapa wasingeweza kutufunga,”amesema.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Buigiri
Mhe Kenneth Yindi ambaye ndiye muandaaji wa mashindano hayo amesema
ataendelea kuandaa mashindano mbalimbali ya Michezo wilayani humo ili
kukuza vipaji vya vijana kwani Michezo imekua ni ajira kubwa
iliyobadilisha maisha ya vijana wengi.
” Mhe DC tunakushukuru sana kwa kufika
pamoja na kufanikisha mashindano haya bado tunakabiliwa haswa na uhaba
wa viwanja pamoja na vifaa vya Michezo, tuwaombe Serikali kuwekeza Kwa
nguvu pia huku vijijini ambapo tunaamini kuna vipaji vingi,” amesema Mhe
Yindi.
Katika fainali hiyo iliyohudhuriwa pia na
Mbunge wa Jimbo la Chilonwa,Joel Mwaka (CCM),Buigiri Mission waliibuka
na ushindi wa Penalti 4-1 dhidi ya Songambele mara baada ya dakika 90
timu hizo kutoka sare ya kutofungana.
Aidha Wachezaji wote wa timu nane
zilizoshiriki mashindano hayo wameweza kupatiwa Bima za afya 159 kwa
kila mchezaji aliyeshiriki.
Bima hizo za Shirika la CHF ambazo Diwani
wa Kata ya Buigiri Mhe.Kenneth Yindi ameweza kuwapatia ili ziweze
kuwalinda katika afya zao hivyo michezo ni Afya.
Jina la mashindano hayo,Buchimwe ni
muunganiko wa herufi za mwanzo za vijiji vitatu vilivyopo katika Kata ya
Buigiri ambavyo ni Chinangali 2,Buigiri na Mwegamile.
0 comments:
Post a Comment