METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, June 17, 2019

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AKUTANA NA WAWEKEZAJI TOKA UTURUKI

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akizungumza na
ujumbe wa wafanyabiashara toka nchini Uturuki. Pembeni yake ni Balozi wa
Uturuki nchini Mhe Ali Davutaglu

Wafanyabiashara wakimsikiliza kwa makini akiwaeleza kuhusu faida za
kuwekeza nchini

Balozi wa Uturuki akimkabidhi Waziri wa Viwanda zawadi ya mojawapo ya
bidhaa zinazotengenezwa Uturuki kwa niaba ya ujumbe wa wafanyabiashara

Mheshimiwa Innocent Bashungwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara
pamoja na balozi wa Uturuki

………………..

Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amekutana na ujumbe wa
wafanyabiashara toka nchini Uturuki katika ofisi za Kiuo cha Uwekezaji
(TIC).

Ujumbe huo ulioongozwa na balozi wa Uturuki nchini Mheshimiwa Ali
Davutaglu ulihusisha wafanyabiashara wa sekta za ujenzi, utalii, chakula na
viwanda mbalimbali.

Wafanyabiashara hao walielezea sifa ya Tanzania kuwa na amani kama kivutio
cha wao kutaka kuwekeza nchini na kusema wangependa kufungua ofisi
itakayokuwa kiungo baina ya wafanyabishara wa Uturuki na wale wa Tanzania.

Mheshimiwa Bashungwa amewahakikishia wafanyabiashara hao kwamba Tanzania ni nchi salama na yenye mazingira rafiki kwa wawekezaji akiahidi kuhakikisha Wizara ya Viwanda na Biashara ikishirikiana kwa ukaribu na taasisi nyingine za Serikali itaharakisha taratibu zote zinazotakiwa ili waanze uwekezaji wao mapema iwezekanavyo.

Pia aliahidi kuwakutanisha na wafanyabiashara wengine nchini ili wapate kufahamiana na kubadilishana ujuzi.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com