Na
George Binagi-GB Pazzo, BMG
Serikali kupita Wizara ya Madini, imetishia kuufunga mgodi wa
dhahabu wa Acacia North Mara uliopo Nyamongo wilayani Tarime, kutokana na
kutiririsha maji machafu hadi katika makazi ya wananchi wanaozunguka mgodi huo.
Waziri wa Madini, Doto Biteko alitoa onyo hilo jana Machi 05,
2019 alipofanya ziara katika mgodi huo akiambatana na Kamati ya Ulinzi na
Usalama Mkoa Mara, Wilaya Tarime pamoja na Maafisa mbalimbali kutoka Wizara
hiyo.
Alisema Septemba 07, 2018 Rais Dkt. John Pombe Magufuli
alipofanya ziara katika eneo la Nyamongo wananchi walilalamikia mgodi huo kutiririsha
maji machafu hadi kwenye makazi yao ambapo Kamati Maalum kutoka Wizara ya Madini
kwa kushirikiana na Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais inayoshughulikia
Mazingira na Muungano iliundwa kuchungumza malalamiko hayo na kubaini kwamba
yalikuwa ya kweli.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akifafanua jambo baada ya kutembelea maeneo yanayolalamikiwa na wananchi kuwa yanatiririsha maji machafu katika mgodi wa Acacia North Mara wilayani Tarime.
Wananchi wa Nyamongo wilayani Tarime mtaro ambao umeanza kuchimbwa ili maji machafu yasitiririke kuelekea kwenye makazi yao.
0 comments:
Post a Comment