Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akisalimiana na Balozi wa Denmark Nchini Einar Jensen walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwake Februari 13, 2019 Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akizungumza jambo na balozi wa Denmark Einar Jensen alipokutana naye kuzungumza masuala ya uwekezaji nchini, Februari 13, 2019 Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Denmark Nchini Bw. Einar Jensen pamoja na wageni alioambatana nao mara baada ya kikao hicho.
NA.MWANDISHI
WETU
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki
amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Dernmark nchini Einar Jensen juu
ya masuala ya maboresho ya mazingira ya biashara pamoja na uwekezaji nchini.
Mazungumzo
hayo yamefanyika hii leo Februari 13, 2019 katika Ofisi yake Jijini Dodoma kwa
lengo la kujadili na kuona namna bora ya kuimarisha masuala ya uwekezaji nchini
kwa kuzingatia fursa zilizopo katika sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Mifugo na
Uvuvi.
Alimtaka
balozi kuendelea kuona fursa na kuzitumia hususan katika kuwekeza kwenye
viwanda hasa vya nguo, mazao ya biashara pamoja na kilimo kwa kuwa ndiyo maeneo
yenye fursa nyingi pamoja na kuleta chachu ya ukuaji wa viwanda nchini.
“Ni vizuri
kuendelea kuimarisha mazingira ya biashara ili kuendelea kuvutia wawekezaji
hasa maeneo ya kilimo na viwanda vya nguo kwa kuwa vinatija katika ukuaji wa
uchumi,”Alisitiza Kairuki
Aidha
aliendelea kumpongeza balozi huyo kwa kutumia muda wake kumtembelea ofisi kwake
kwa lengo la kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masula ya kuboresha
mazingira ya biashara pamoja na kuendelea kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia
baina ya nchi hizo mbili.
“Kipekee
nikushukiuru kwa kutembelea ofisi yetu na hii ni ishara nzuri
yakuimarisha mahusiano ya kidiplomasia ambayo yatasaidia Serikali yetu
kuendelea kuwa na mazingira rafiki kwa wawekezaji kuzingatia fursa
zilizopo katika maeneo mengi ikiwemo; Sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi
nchini”alisisitiza kairuki
Kwa upande
wake Balozi wa Dernmark nchini, Einar Jensen aliahidi kuendelea kushirikiana na
Serikali katika maeneo ya maboresho ya biashara ikiwa ni pamoja na kuwekeza
nchini katika sekta mbalimbali
“Nimefarijika
kukutana na Waziri mwenye dhamana ya uwekezaji na kupata muongozo wa masuala ya
uwekezaji nchini na kuendelea kutumia fursa zilizopo Tanzania na ninaahidi
kutoa ushirikiano ili kuleta chachu katika ukuaji wa viwanda kwa kuleta
wawekezaji katika sekta mbalimbali,”alisistiza Jensen.
=MWISHO=
0 comments:
Post a Comment