METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, February 1, 2019

SHIMIWI wahimiza mabonanza kuimarisha afya



Na Mwandishi Wetu, Dodoma

SHIRIKISHO la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala wa Serikali, na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), imehimiza ushiriki wa mabonanza ya michezo mbalimbali kwa Watumishi wa Umma ili kuboresha afya zao.

Mwenyekiti wa SHIMIWI, Daniel Mwalusamba amesema jana jijini Dodoma, katika mkutano wa wenyeviti na Makatibu uliofanyika kwenye ukumbi wa Naibu Waziri wa Fedha katika jengo la Hazina.

Mwalusamba amesema kwa sasa serikali inahimiza ujenzi wa viwanda, ili tufikie uchumi wa kati, ambapo Watumishi wa Umma wanatakiwa kuunga mkono hatua hiyo iliyotangazwa na Mhe. Rais John Pombe Magufuli.

“Tuondokane na zana ya SHIMIWI kuwa imekufa kwani hili ni Shirikisho la michezo ambalo lipo kihalali na linaendeshwa kwa utaratibu, na mapendekezo yote yapo kisheria,” amesema Mwalusamba.

Hatahivyo, Mwalusamba amesema SHIMIWI inakumbwa na changamoto za klabu kwa kushindwa kwenda na katibka kwa kufanya chaguzi zake kwa wakati, ikiwa ni kufuata katiba iliyopo.

“Hairihusiwi kikatika kwenye mkutano mkuu kuingia na viongozi ambao hawajachaguliwa kihalali na kukaa kwa muda mrefu, kwani ni kinyume na katiba yetu ya Shimiwi na pia katiba Mama ya serikali, ambayo imeweka wazi juu ya muda wa ukomo wa uongozi,”

Amesema ni kinyume na katiba na viongozi wa shimiwi wanaweza kwenda kwa Katibu Mkuu wa wizara husika, na sasa SHIMIWI itafanya ukaguzi na kugundua klabu iliyo na uongozi uliomaliza muda, hali kadhalika katiba za klabu zinapitishwa na baraza, na sio kikundi kinachojiendesha chenyewe bila kufuata katiba.

Ameagiza klabu sugu zikafanye chaguzi zao ili kuepusha mgogoro, kwani  SHIMIWI imekuwa mfano wa kuigwa kwa kufuata taratibu tofauti na mashirikisho mengine.

Mwisho                                                                                                                              
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com