Kikosi
kazi kinachoshughulikia rasimu ya
muswada wa sheria ya ardhi ya Kilimo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada
ya kukamilisha kazi hiyo iliyokuwa inafanyika katika ukumbi wa chuo cha
wakulima Bihawana hivi karibuni.
Na Bashiri Salum, Dodoma
Sehemu kubwa ya ardhi inayotumika
kwa shughuli za kilimo nchini haitambuliki kama ni ardhi ya kilimo kisheria
hivyo kuwa ni chanzo cha migogoro hasa vijijini.
Akiongea wakati wa kikao kazi cha
maandalizi ya sheria ya kuanisha kulinda na kusimamia matumizi ya ardhi ya
kilimo kilichofanyika katika ukumbi wa
chuo cha wakulima Bihawana hivi karibuni, Mkurungenzi wa Idara ya
Usimamiaji na Mipango ya Ardhi Bwana Paulo Tarimo amesema sehemu ya ardhi
inayotumiwa kwa shughuli za kilimo imekuwa ikipangiwa matumizi mengine hivyo
kuwa chanzo cha migogoro hapa nchini.
Aidha tafiti za kisayansi
zinaonesha kwamba zipo ikolojia mbalimbali za kilimo hapa nchini lakini ardhi inayofaa kwa kilimo imekuwa ikipangiwa
matumizi mbalimbali bila kujali mahitaji ya ardhi ya kilimo kwa matumizi ya
sasa na ya baadaye alisistiza Bwana Tarimo.
hata hivyo amesisitiza kwamba
idadi ya watu imekuwa ikiongezeka kwa kasi lakini ardhi haiongezeki, hivyo jitihada
za dhati zinatakiwa kuchukuliwa ili
kuanisha kulinda na kusimamia ardhi hiyo kwa manufaa mapana ya
kuimarisha uzalishaji na uwekezaji katika kilimo.
Aidha amebainisha kwamba Wizara ya Kilimo kupitia
Idara ya Mipango na Matumizi ya Aridhi
ya Kilimo imekutana mara kadhaa kuandaa
rasimu ya sheria ya kuainisha, kulinda na kusimamia matumizi ya ardhi ya kilimo
ili kupunguza migogoro ya aridhi ambayo imekuwa ikisababishwa kwa kiasi kikubwa
na uwepo wa matumizi mengine yasikuwa ya kilimo katika ardhi hiyo.
'migogoro mingi ya ardhi ipo vijijini ambayo inasababishwa na muingiliano
wa matumizi ya ardhi ya kilimo na matumizi mengine yasiyokuwa na kilimo hivyo
sheria hiyo itasaidia ardhi ya kilimo kutambuliwa kuwa ni maalum kwa shughuli za kilimo."
Hata hivyo ameendelea
kueleza kwamba sheria hii itakuwa na
manufaa kwa wakulima na wawekezaji kwa sababu italinda rutuba ya udongo na kuleta uendelevu wa
matumizi ya ardhi hiyo kwa kuwa watumiaji watalazimika kuitumia ardhi kwa misingi ya kanuni za kilimo bora zitakazokuwa
zimeainishwa.
''Sehemu kubwa ya ardhi
inayotumika kwa shughuli za kilimo haitumiki kwa kupewa matunzo ya kutosha ili
kuiwezesha kutumika kwa muda mrefu bila ya kuathiri rutuba na ubora wake''.
aliendelea kueleza Bwana Tarimo.
sheria hii ni muhimu kwa kuwa itasaidia kuwekwa
katika madaraja yatakayoainisha idadi na uwezo wa kimtaji na kiteknolojia wa
wakulima wadogo, wa kati na wakubwa. Hii itaongeza tija na ufanisi katika
kusimamia na kuratibu uendelezaji wa rasilimali ardhi ya kilimo nchini.
hata hivyo uaandaaji wa rasimu ya muswada huo ulitokana
na marekebisho ambayo yalitolewa awali
na kikao cha baraza la mawaziri kilicho fanyika hivi karibuni.
Aidha kikao hicho kilijumuisha wadau mbalimbali ambapo
matokeo ya kikao kazi hicho yatajadiliwa katika ngazi mbambali kabla ya
kupelekwa katika baraza la mawaziri.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment