Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo (wa pili toka kulia) akiwa
pamoja na mwenye shamba hili Alenx Ndenge (kulia) pamoja na wataalamu
mbalimbali wakiangalia namna viwavijeshi vamizi wanavyoanza kushambulia mimea
ya mahindi wilayani Nkasi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim
Wangabo (wa pili toka kulia) akiwa pamoja na mwenye shamba hili Alenx Ndenge
(kulia) pamoja na wataalamu mbalimbali wakiangalia namna viwavijeshi vamizi
wanavyoanza kushambulia mimea ya mahindi wilayani Nkasi.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo
amewaagiza maafisa ugani wote wa mkoani humo kuhakikisha wanawafikia wakulima
kwenye mashamba yao na kuwapa elimu ya kukabiliana na wadudu aina ya
viwavijeshi vamizi ambao wanaonekana kuanza kuleta athari katika wilaya ya
Nkasi.
Amesema kuwa wakulima wengi hawana elimu ya
kukabiliana na wadudu hao hasa kujua aina ya dawa ya kutumia ili kuwaua na
wasiendelee kuharibu mazao na kuongeza kuwa ni wakati wao sasa maafisa ugani
kufanya kazi ya kuwasaidia wananchi kupata matokeo bora ya mavuno kwa kutoa
elimu ya kukabiliana na wadudu waharibifu na magonjwa.
“Kitu cha kufanya ni maafisa ugani wote na maafisa
kilimo wote washuke kwenda kwenye mashamba, wakague na kutoa ushauri wa moja
kwa moja, dawa zipo zinapatikana wanaanzia dawa gani inayofuata ni ipi, ili
tuweze kuwasaidia wakulima waweze kuokoa haya mahindi, DC hawa watu wasimamiwe
washuke asibaki mtu kwenye ofisi zao,” Alisisitiza.
Ameyasema hayo baada ya kuona athari ya viwavi
jeshi alipotembelea shamba la mkulima wa mahindi Alex Ndenge katika ziara yake
ya kuangalia maendeleo ya kilimo kwa wakulima na changamoto wanazokabiliana
nazo ikiwemo upatikanaji wa pembejeo pamoja na mashambulizi ya wadudu na
magonjwa ya mazao Wilayani Nkasi.
Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Mkoa wa Rukwa Ocran
Chengula alifafanua namna ya kupambana na wadudu hao na kutoa tahadhari kwa
wakulima kuwa na tabia ya kupanda kwa kipindi kimoja na sio kupishana kwani
hali hiyo hupelekea wadudu hao kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine ili
kufuata mimea teke.
“Kuna sumu nyingine ukipiga inakuwa kwenye mmea,
kwasababu huyu (mdudu) anatoa kinyesi kwahiyo ile sumu inaingia kwenye mmea
kwahiyo anapokula anapata madhara anakufa, kwahiyo katika hatua za kwanza
tunashauri (dawa aina ya) Duduba na hatua ya pili tunashauri dawa inaitwa
“systemic” japo zina majina tofauti tofauti ni amjina ya kibiashara ila itumike
hiyo baada ya kuona kwamba wameshaanza kutoa huu uchafu” Alieleza.
Kwa mujibu wa Afisa kilimo wa halmashauri ya wilaya
ya Nkasi Emanuel Sekwao amesema kuwa viwavijeshi vamizi hao wameshaathiri kwa
asilimia 2 mpaka 5 kutegemea eneo lakini bado haijafikia hatua ya wadudu hao
kuharibu mimea kiasi cha kushindwa kuzaa.
Katika kipindi cha mwaka 2018/19 mkoa
unalenga kulima jumla ya hekta 599,345.45 za mazao mbalimbali,
kati ya hizo hekta517,482.15 ni za mazao ya chakula na hekta 81,863.3 za
mazao ya biashara. Kutokana na eneo hilo mkoa unategemea kuzalisha jumla
ya tani 1,817,171.84 za mazao ya chakula na biashara.
Katika
kiasi hicho tani 1,680,701.6 ni za mazao ya chakula na
tani 136,470.25 ni za mazao ya biashara.
0 comments:
Post a Comment