METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, January 11, 2019

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUJITOSHELEZA KWA SUKARI NCHINI





Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba yupo kwenye ziara ya kikazi ya siku nane (8) kuanzia tarehe 07 Januri mpaka tarehe 14 Januari 2019 kwenye Mikoa ya Kilimanjaro, Morogoro na Pwani yenye Lengo la kuhamasisha uzalishaji na tija wa Miwa na Sukari  ili kumaliza tatizo la upungufu wa Sukari Nchini.

Naibu Waziri huyo amesema kuwa Tanzania ina miaka 57 ya Uhuru lakini kama Taifa halijawahi kujitosheleza kwa Sukari badala yake inaagizwa toka nje ya nchi wakati uwezo wa kuzalisha upo, ardhi na Rasilimali watu zote zipo hivyo jambo hilo linapoteza fedha za kigeni na ajira kwenda nchi zingine.

Alisema kuwa Serikali imeazimia kubaini sababu na changamoto zinazokabili sekta ya Sukari, wadau, Wakulima wadogo na wakubwa wa miwa na wawekezaji wa viwanda vya sukari nchini ili kwa pamoja kuwa na mkakati kabambe wa kukamilisha upungugu huo ndani ya muda mfupi.

Kwa sasa Mahitaji ya Sukari nchini yanakadiriwa kufikia zaidi ya Tani 670,000 Mts kwa pamoja ya Sukari ya Mezani na viwandani. Sukari ya Mezani ni Tani 515,000 na Sukari ya Viwandnai Tani 155,000 Mts.

Uwezo wa Viwanda vya ndani ni kuzalisha ni Tani 350,000 Mts na kuwa na upungufu wa Tani 320,000 Mts za Mezani na Viwandani kiasi ambacho kinaagizwa kila mwaka toka nje ya nchi.

Katika ziara hiyo Mhe Mgumba amewahimiza wakulima kuzalisha zaidi na kuwaomba wawekezaji waliopo kupanua uwezo wa viwanda vyao ili kuongeza uzalishahi na kuwahamasisha pia wakulima kuongeza uzalishaji wa kilimo na kuwaomba wawekezaji wengine wa ndani na nje ya nchi kutumia fursa hiyo kuwekeza nchini kwa sababu soko lipo na mazingira ya Biadhara yanaendelea kuboreshwa kila siku.

Katika Ziara hiyo Mh Mgumba aliambatana na  Mhe Joseph Kakunda ambaye ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji mwenye dhamana ya kusimamia sekta ya viwanda nchini.

Baada ya ziara hiyo watatembelea pia Mkoani Kagera kwa lengo kama hilo ili kuweza kufahamu changamoto za wadau wote katika sekta hiyo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com