Waziri
wa Madini, Doto Biteko akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Uranium
One Holdings N.V, Vladimir Hlavinka mara baada ya kuwasili ofisini kwake kwa
mazungumzo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra, Fredrick
Kibodya.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akimsikiliza Makamu
wa Rais wa kampuni ya Uranium One Holdings N.V, Vladimir Hlavinka akielezea nia
yao ya kutaka kuwekeza katika sekta ya madini nchini wakisubiri uwekezaji wao
katika masuala ya uranium uliositishwa kwa muda.
Na Nuru Mwasampeta, Dodoma
Waziri
wa Madini, Doto Biteko ameitaka kampuni
inayojishughulisha na uchimbaji wa madini
ya uranium katika mto Mkuju ulioko mkoani Lindi ya Uranium One kutokusita kuwasiliana naye pindi wanapokutana
na changamoto katika utekelezaji wa mradi wao.
Aliyasema
hayo jana tarehe 15 Januari, 2019 katika
kikao chake na watendaji wa kampuni hiyo kilichofanyika ofisini kwake jijini
Dodoma.
Aidha,
Biteko alisema kuwa maombi yote ya leseni kubwa za uchimbaji wa madini
zinawasilishwa katika baraza la Mawaziri ili kuweza kuridhiwa baada ya
wawekezaji kuonesha nia na kuwasilisha maombi ya leseni hizo.
Biteko
alikiri kuwa anao uelewa wa kile kinachoendelea katika uwekezaji huo kutokana
na ushirikishwaji alioupata kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Madini, Angellah
Kairuki kupitia vikao mbalimbali alivyoshiriki.
Akizungumzia
lengo la ujio wao katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Uranium
One, Frederick Kibodya alisema ni kuelezea maendeleo waliyofikia katika
uwekezaji huo pamoja na kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Madini.
Alisema,
uteuzi huo umelenga katika kukuza sekta ya madini ikiwa ni pamoja na mradi wa
uchimbaji wa madini ya uranium, “Tunaimani kubwa kwako na tunamshukuru Mungu
kwa kukupa nafasi hii” alisema Kibodya.
Akizungumzia
uwekezaji uliofanyika mpaka sasa katika mradi huo alisema ni kiasi cha dola za
kimarekani Milioni mia mbili ($200mil) kutoka mradi ulipoanza mwaka 2009.
Akizungumzia
manufaa ya mradi huo Kibodya alisema ni
pamoja na kusaidia katika kukuza teknolojia nchini. Alisema madini hayo
yakichimbwa yanatumika katika kuzalisha umeme ambayo ni teknolijia mpya nchini.
Mradi
utasaidia katika kuongeza ajira nchini. Aliendelea kufafanua kuwa kwa kipindi
cha ujenzi wa mradi wanatarajia kuajiri watanzania 1600 kwa kipindi cha miezi
kumi na nane.
Aidha,
alibainisha kuwa kutakuwepo na uzalishaji wa ajila zisiso rasmi kiasi cha watu
4500 wakati wa ujenzi na 2300 pindi uzalishaji utakapoanza.
Alisema,
mradi utasaidia katika kuhamisha utaalamu kutoka kwa wawekezaji kwenda kwa
wazawa na mradi umelenga katika kutoa elimu ya ajira na utaalamu kwa wazawa.
Pia
Kibodya alisema, mradi unatarajia kuliingizia taifa pato la kiasi cha dola za
kimarekani milioni 220 kama kodi kwa mwaka, kiasi ambacho kitakuwa kikibadilika kadri uzalishaji
unavyoongezeka.
Mradi
wa uchimbaji madini ya uranium katika mto Mkuju unafanywa kwa ushirikiano baina
ya Serikali ya Tanzania na Mbia wa kampuni ya Mantra anayejulikana kama
Rosatom.
0 comments:
Post a Comment