Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar katika eneo la Pagali Shehia ya Mikoroshini Chake Chake Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga
makofi kuashiria zoezi la uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa
makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar limekamilika, mwingine pichani ni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud, makazi hayo
yanajengwa katika eneo la Pagali Shehia ya Mikoroshini Chake Chake Pemba.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar katika eneo la Pagali Shehia ya Mikoroshini Chake Chake Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutumia Vikosi vyake
katika ujenzi wa miradi ya maendeleo.
Makamu wa Rais ametoa pongezi zake leo wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe
la msingi wa ujenzi wa nyumba ya makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
katika eneo la Pagali Shehia ya Mkoroshoni Chake Chake Pemba.
Hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa nyumba ya makazi ya
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar ni sehemu ya shamra shamra za miaka 55 ya
Mapinduzi Takatifu ambayo kilele chake itakuwa Jumamosi tarehe 12 Januari,
2019.
“Sote tutakumbuka kuwa wakati wa kupigania
uhuru wetu Chama cha Afro Shirazi Party (ASP) kiliwaahidi wananchi wake
kuwajengea makaazi bora yenye heshima ya utu. Ahadi za ASP zimerithiwa na Chama
cha Mapinduzi na ndio maana leo hii tupo hapa kushuhudia uwekaji wa jiwe la
msingi la makazi bora ya mwananchi mwenzenu, kiongozi wetu, Makamu wa Pili wa
Rais”. Alisema Makamu wa Rais.
Ujenzi huo wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar utagharimu
kiasi cha shilingi bilioni 1.6 za kitanzania.
Kwa Upande mwingine Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe.
Mohammed Aboud Mohammed amesema Serikali imeweka umuhimu katika kujenga makazi
ya watumishi wake pamoja na Ofisi.
0 comments:
Post a Comment