Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliye kuwa akimueleza
juu ya ujenzi wa mfereji wa mto Ngo’mbe, wakati wa ziara yake ya
kukagua miundo mbinu ya kukabili maafa ya mafuriko mkoani Dar es Salaam. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza, Bibi, Nuru Damson, mkazi wa Dar es Salaam, aliye kuwa akimueleza jinsi ujenzi wa mfereji wa mto Ngo’mbe, ulivyowasaidia kutopata athari za maafa ya mafuriko wakati wa ziara yake ya kukagua miundo mbinu ya kukabili maafa ya mafuriko mkoani Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akioneshwa ujenzi wa miundombinu ya kukabili maafa ya mafuriko mkoani Dar es saaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wakati wa ziara yake ya kukagua miundo mbinu hiyo mkoani humo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama amefanya ziara ya siku moja mkoani Dar es salaam, lengo la
ziara hiyo ni kukagua miundo mbinu ya kukabiliana na maafa ya mafuriko pamoja
na kutaka kujua mikakati ya kamati ya Usimamizi wa menejimenti ya maafa mkoani
humo ya kukabiliana na maafa hayo.
Katika
ziara hiyo Waziri Mhagama emetembelea wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam
hususan katika maeneo ambayo mkoa huo umeboresha miundo mbinu ya kukabiliana na
maafa ya mafuriko. Maeneo hayo ni Jangwani, Mto Mbezi, Mto Ng’ombe, Mto Bungoni
na mfereji wa Mtoni kwa Azizi Ally.
Pamoja
na kuridhishwa na jitihada zilizofanywa na mkoa wa Dar es salaam za kuboresha
miundombinu ya kukabiliana na maafa ya mafuriko, pia na mikakati ya kukabiliana
na maafa hayo waliyomueleza, Waziri Mhagama ametoa maagizo 5 kwa kamati ya Usimamizi
wa menejimenti ya maafa ya mkoa huo kuyatekeleza ili menejimenti ya maafa ya mafuriko mkaoni
Dares salaam iwe endelevu.
“Nimeridhishwa na juhudi zilizofanywa na serikali kuu chini ya
uongozi wa Dkt.Joh Pombe Magufuli za kuboresha miundo mbinu ya kakabiliana na
maafa ya mafuriko, na nimeona jinsi serikali ya ngazi ya mkoa na wilaya zote
zinavyo jitahidi kujenga uwezo wa kuzuia,
kujiandaa na kukabiliana na maafa. Pamoja na jitihada hizo ninge penda
kuishauri na kuielekeza kamati na Mkuu
wa mkoa ayasimamie maelekezo yangu.” Amesisitiza Mhagama
Mhagama
ameiagiza Kamati ya Usimamizi wa menejimenti ya maafa kusimamia suala la uharibifu
wa mazingira hususani maeneo ya mito na mabondeni kwa mujibu wa sheria ya
menejimenti ya maafa ya mwaka 2015. Aidha alifafanua kuwa Maafa mengi ya
mafuriko mkoani humo yanatokana na uharibifu wa mazingira unaochangiwa na ujenzi
katika maeneno yasiyo stahili kama kingo za mito na mabondeni hali
ambayo huzuia maji kutiririka na kusababisha mafuriko.
Aidha
Mhagama ameitaka kamati hiyo kusimamia
suala la usafi wa mitaro, mifereji na mito iliyopo jijini
Dares salaam, ambayo hujaa maji wakati wa msimu wa mvua kutokana na uchafu na takataka zilizotupwa katika
mifereji na mitaro hiyo hali ambayo husababisha maji kushindwa kutirirka
kuelekea baharini na hatimaye mitaro hiyo hujaa na kusababisha mafuriko.
Ameitaka
kamati hiyo kuwasiliana na sekta nyingine zenye miundmbinu katika mitaro na mifereji
inayojengwa na kuondoa miundo mbinu hiyo ili uboreshaji wa miundo mbinu hiyo
kuwa wa ufanisi. Mhagama alibainisha kuwa Mkoa umefanya juhudi nzuri za kujenga mitaro na mifereji
lakini ndani ya miundo mbinu hiyo kuna miundombinu mingine kama vile mabomba
ya maji safi, hivyo,
sekta nyingine husika hazina budi kushrikishwa na kuhakikisha miundo
mbinu hiyo inatolewa ili kulifanya zoezi la kuboresha miundombinu ya maafa ya
mafuriko linakuwa bora na ufanisi.
Kamati
imetakiwa kuhakikisha miradi yote inayolenga kuboresha miundombinu ya
kukabiliana na maafa ya mafuriko ndani ya mkoa wa Dar es salaam inashirikiana
katika hatua ya kupanga utekelezaji wake. Mhagama amefafanua kuwa Mkoa una
miradi mingi ya kuboresha miundo mbinu ya kukabiliana na maafa hivyo ni vyema
miradi hiyo ikae pamoja ili kujua ni namna gani ya kutekeleza malengo yake
hususani kujua miundo mbinu husika inawekwa wapi bila kuathiri utekelezaji wa
mradi mwingine.
Mhe.Mhagama
ameitaka kamati kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya sheria ya menejimenti ya
maafa ya mwaka 2015. Amebainisha kuwa kila mmoja katika jamii analojukumu la
kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na maafa, hivyo jamii ikiwa na elimu ya
kutosha juu ya menejimenti ya maafa hususani ya mafuriko jamii haitapata athari
kubwa za uharibifu wa mali na vifo vitokanavyo na maafa ya mafuriko.
Awali akieleza mikakati iliyopo ya
kukabibiliana na maafa katika mkoa wa Dar es salaam, Mkuu wa mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda alifafanua kuwa mkoa wa Dar es salam umekuwa ukitumia
fedha nyingi wakati wa kurejesha hali ya miundo mbinu iliyoathirika kutokana na
maafa ya mafuriko ambapo kwa mwaka 2011, kiasi cha shilingi bilioni Nne na nusu
kilitumika kurejesha hali ya miundo mbinu ya barabara iliyoharibika.
“Mkoa
wa Dar es salaam tuna mito mikubwa saba ambayo inatiririsha maji kuelekea baharini, na mito midogo midogo
mingi, sisi kama mkoa tumejipanga kuhakikisha mito hiyo ambayo hujaa maji na
kusababisha maafa ya mafuriko tunaidhibiti. Kupitia Benki ya Dunia tunao mpango
wa kuchukua picha za anga la mkoa wa Dar es salaam, lengo ni kujua nyumba
zilizo kando ya mito hiyo na idadi ya
mito na kujipanga jinsi ya kuhakikisha kuwa haileti athari ya mafuriko”amesema Makonda.
Naye
mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Menejimenti ya Maafa ya Mkoa wa Dar es
Salaam kwa mujibu wa sheria ya maafa ya menejimenti ya maafa mwaka 2015, Katibu
Tawala wa mkoa wa Dar es Salaam, alimhakikishia Waziri Mhagama kutelekeleza
maagizo hayo kwa wakati kwa kuwa tayari kamati ya Usimamizi wa menejimenti wa
maafa ya mkoa imesimamaia uundwaji wa kamati za Usimamizi wa menejimenti ya
maafa katika Halmashauri zake tano hai itakayo saidia ufuatiliaji wa masuaa ya
maafa mkoani humo.
Katika
ziara hiyo Waziri Mhagama aliambatana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera
na Uratibu), Profesa. Faustin Kamuzora,
Mkurugenzi wa Idara ya uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy
Matamwe, Mkuu wa wila ya Ilala, Temeke, na Kinondoni pamoja na wajumbe wa
Kamati ya Usimamizi wa Menejimenti ya Maafa ya Mkoa wa Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment