Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akifanya mazungumzo
na watendaji wakuu wa kampuni ya utengenezaji na wasambazaji wa mbolea
YARA katika mkutano uliofanyika Mjini Kigali nchini Rwanda jana tarehe 7
Septemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akiagana na watendaji wakuu wa kampuni ya utengenezaji na wasambazaji wa mbolea
YARA mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi katika mkutano uliofanyika Mjini Kigali nchini Rwanda jana tarehe 7
Septemba 2018.
Na Mathias Canal,
Kigali-Rwanda
Waziri wa kilimo Mhe Dkt
Charles Tizeba jana tarehe 7 Septemba 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na
watendaji wakuu wa kampuni ya utengenezaji na wasambazaji wa mbolea YARA.
Katika kikao hicho
kilichofanyika katika ulumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kigali Convertion
Centre uliopo mjini Kigali nchini Rwanda Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni
pamoja na bei ya mbolea hiyo ikiwa ni pamoja na maswala mazima ya Ubora wake.
Mbolea za YARA zimegawanyika
katika makundi makuu matano Yara Mila: Kundi hili lina aina
za mbolea zenye madini makubwa matatu yaani NPK (Nitrogen, Phosphorus,
Potassium), Yara Liva: Kundi hili lina aina za mbolea zenye asili
ya Calcium Nitrate ambazo ni kama vile
Nitrabor, Tropicoti na Calicinite, Yara Bela: Kundi hili ni Kundi
lenye mbolea zenye asili ya Ammonium Sulphate Nitrate, zina Nitrojen na Sulphur
ambazo ni Sulfan, Yara Vita: Kundi hili ni la
mbolea zile zenye madini yanayohitajika kwa kiwango kidogo na mmea (MicroNutrients)
lakini muhimu katika ukuaji wa mmea sambamba na Yara Vera: Kundi
la tano na la mwisho ni mbolea za UREA.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment