METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, July 14, 2018

MD KAYOMBO AVITAKA VYAMA VINAVYOSHIRIKI UCHAGUZI MDOGO KUZINGATA KANUNI NA TARATIBU ZA UCHAGUZI

Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi mdogo wa marudio Kata ya Kimara Ndg John Lipesi Kayombo amevitaka vyama vitakavyoshiriki uchaguzi wa marudio kuzingatia kanuni na taratibu za uchaguzi kwa mujibu wa sheria.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya kata ya kimara mara baada ya kupokea fomu za majina ya wagombea wa nafasi ya udiwani katika kata ya kimara kutoka katika vyama mbalimbali vya siasa.

Kayombo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo amesema kinachofanyika sasa baada ya kupata majina ya wanaoingia katika kinyang'anyiro cha nafasi ya udiwani ni kupitia taarifa zao kama wamekidhi vigezo kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi .

Na endapo watakidhi vigezo kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi majina hayo yatatangazwa tayari kwa kuanza kampeni za kujinadi kwa wananchi ili kuweza kuchaguliwa au kupigiwa kura katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 12/08/2018

Rai yangu  kwa wagombea na wananchi kwa ujumla kaendesheni siasa za Kistaarabu zisizo za matusi wala vurugu kwa upande wa vyama vyote hatutavumilia aina yoyote ya vurugu, kanuni na taratibu za uchaguzi zizingatiwe alisistiza Kayombo

Ikumbukwe kuwa uchaguzi huo mdogo wa Kata ya Kimara ni wa marudio  kutokana na aliyekuwa Diwani wa kata hiyo kwa Tiketi ya Chedema kuamua kujiuzuru .

MWISHO.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com