Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza kwenye kikao kazi kilichowakutanisha watendaji wa Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Maruku, Taasisi ya utafiti wa kahawa (TACRI) na Uongozi wa chuo cha mafunzo ya kilimo MARUKU katika kijiji cha Butairuka Kata ya Maruku Wilayani Bukoba vijijini, Leo 13 Julai 2018. (Picha zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba mbegu za maharege zinazofanyiwa utafiti na Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Maruku, wakati akiwa katika ziara ya kikazi katika kijiji cha Butairuka Kata ya Maruku Wilayani Bukoba vijijini, Leo 13 Julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza kwenye kikao kazi kilichowakutanisha watendaji wa Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Maruku, Taasisi ya utafiti wa kahawa (TACRI) na Uongozi wa chuo cha mafunzo ya kilimo MARUKU katika kijiji cha Butairuka Kata ya Maruku Wilayani Bukoba vijijini, Leo 13 Julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba mbegu za maharege zinazofanyiwa utafiti na Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Maruku, wakati akiwa katika ziara ya kikazi katika kijiji cha Butairuka Kata ya Maruku Wilayani Bukoba vijijini, Leo 13 Julai 2018.
Na Mathias Canal-WK, Bukoba-Kagera
UONGOZI wa Taasisi ya utafiti wa
kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Maruku, Taasisi ya utafiti wa kahawa (TACRI)
umetakiwa kuongeza ufanisi katika utaalamu wao ili kuwanufaisha wakulima kote
nchini kwani kwa sasa Benki ya Tafiti zilizopo hazijatumika ipasavyo.
Wataalamu wa utafiti wamepaswa
kufanya vizuri pia katika eneo la kutangaza tafiti zao ikiwemo Kuongeza ujuzi
katika Utafiti wa Mazao mbalimbali ikiwa ni pamoja na zao la kahawa ili
kuongeza uwezo wa uzalishaji wa miche.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles
Tizeba ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao kazi kilichowakutanisha
watendaji wa taasisi hizo za utafiti sambamba na uongozi wa chuo cha mafunzo ya
Kilimo MARUKU katika kijiji cha Butairuka Kata ya Maruku Wilayani Bukoba
vijijini.
Waziri huyo wa kilimo aliwasihi
watafiti hao Kuendelea kufanya juhudi kubwa kuandika miradi mbalimbali (Reseach
Proposals) kwa ajili ya kusaidia shughuli za uendelezaji wa utafiti kwani
bajeti ya serikali pekee haiwezi kutosha kukamilisha kila changamoto zinazowakabili.
Alisema wataalamu hao wanapaswa
kufanya tafiti kwa kuendana na matakwa ya sekta ya kilimo na serikali ya
awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
John Pombe Magufuli ili kuongeza tija katika uzalishaji wa Kahawa nchini
sambamba na Mazao mengine.
Aliwasihi kuongeza ushirikiano
ili kuendelea na utafiti kuhusu njia bora za uzalishaji mazao, urutubishaji
udongo, mfumo wa usambazaji wa teknolojia, masoko yenye tija, tathmini ya
uenezaji wa teknolojia na mchango wa matokeo ya utafiti katika kuboresha hali
ya maisha ya wananchi na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Alisema kuwa kituo cha utafiti
wa kilimo kinapaswa kuendelea na juhudi za uzalishaji wa mbegu bora za mazao
mbalimbali kama vile maharage, viazi vitamu, muhogo na mengineyo.
Kituo cha utafiti wa kilimo cha
Maruku (TARI-MARUKU) ni kati ya vituo viwili vya utafiti wa kilimo katika Kanda
ya ziwa ambapo makao makuu yake yapo Ukiriguru-Mwanza ambapo kinatoa mafunzo na
ushauri kwa wakulima na wadau mbalimbali wa kilimo juu ya teknolojia mbalimbali
za kilimo.
Katika hatua nyingine Waziri
Tizeba amemuagiza Mkuu wa chuo cha mafunzo ya kilimo Maruku Ndg Laurent Mathew
Luhembe ndani ya mwaka mmoja kutatua changamoto ya ukosefu wa bweni la chakula.
Aliongeza kuwa chuo hicho
kinapaswa kubuni mbinu mbadala za mapato ikiwa ni pamoja na kujenga kitalu
nyumba (Green House) kwani itasaidia kuongeza kipato mahususi na hatimaye chuo
kujiendesha badala ya kutaka changamoto zote zitatuliwe na serikali.
Aidha, Taasisi hizo za utafiti
ikiwa ni pamoja na Chuo cha Maendeleo ya kilimo Maruku zimetakiwa kuhakikisha
wanatunza ardhi yao ili kuondosha hofu ya uvamizi wa maeneo.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment