Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza alipokuwa akikabidhi vifaa mbalimbali kwa ajili ya misikiti ya Jimbo la Dodoma Mjini
Vifaa mbalimbali vilivyokabishiwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde kwa ajili ya misikiti ya Jimbo hilo.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akimkabidhi vifaa mbalimbali kwa ajili ya misikiti ya Jimbo la Dodoma Mjini Shekhe wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajab
Shekhe wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajab akizungumza katika Hafla ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali vya misikiti ya Dodoma.
Waumini wakiwasikiliza viongozi mbalimbali
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Peter Mavunde amewaomba waamini wa Dini ya kiislamu kuliombea Taifa,Rais Dk.John Magufuli na Viongozi wote wa Serikali ya awamu ya Tano ili waweze kutimiza majukumu yao kwa Haki na Usawa na kuendelea kuwahudumia Watanzania wanyonge.
Mavunde ameyasema hayo leo katika Masjid Gaddafi alipokuwa akikabidhi vifaa mbalimbali kwa ajili ya misikiti ya Jimbo la Dodoma Mjini ambapo Mbunge huyo amegawa Speaker 20 za misikitini,mikeka,mabusati,Mifuko ya Saruji,matofali,tende,maboksi matano ya Juzuu & Misahafu,Jezi,Mipira vyote vyenye thamani ya Tsh 15,000,000 na fedha taslimu kwa Tsh 1,000,000 kwa kikundi cha Vijana cha UWAZAM na kuwataka wanufaika wa Vifaa hivyo kuvitumia kwa madhumuni yaliyokusudiwa.
“Rais wetu pamoja na viongozi wetu wakuu wanafanya kazi nzuri sana ambayo inapaswa kuungwa mkono,tuliombee Taifa na Viongozi wetu ili waendelee kututumikia na kutatua changamoto zetu”Alisema Mavunde.
Aidha akimkaribisha Mh Mavunde,Sheikh wa Mkoa Wa Dodoma Al-ahi Sheikh Mustafa Rajab amemshukuru sana Mbunge Mavunde kwa kuwa mstari wa mbele kushirikiana na Waislamu na kuwataka waamini wa Dini ya Kislamu kumuombea na kumpa ushirikiano muda wote.
0 comments:
Post a Comment