Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* amewaonya wakandarasi wenye tabia ya kutengeneza *Barabara za chini ya kiwango* na kuharibika ndani ya *muda mfupi* jambo linalosababisha *hasara kwa serikali* na usumbufu kwa watumiaji wa *vyombo vya usafiri.*
*RC Makonda* ametoa onyo hilo wakati wa hafla ya *utiaji wa saini kwa Mikataba Nane ya mradi wa matengenezo ya Barabara, Mifereji ya Maji na Culvets* inayotekelezwa na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini *TARURA* yenye tahamani ya zaidi ya *Billion 5.8* ambapo amewataka *TARURA* kuhakikisha *wanasimamia ipasavyo* ujenzi wa barabara hizo.
Aidha *RC Makonda* amezitaja Barabara zitakazojengwa kupitika *mradi* huo kuwa ni pamoja na *Tegeta Nyuki, Msasani, Magomeni Makuti,Migombani, Kimara baruti, Kibanda cha Mkaa, Sheikh Bofu, Kwa Komba, Msigani, Sea clif na Mwananyamala Kisiwani.*
Hata hivyo *RC Makonda* ametoa *wiki mbili* kwa *TARURA* kuhakikisha wakandarasi waliojenga *barabara chini ya kiwango* zinajengwa *upya* kwa *gharama ya mkandarasi* ikiwemo *barabara ya Mabatini* ambapo barabara hizo zitakuwa na *mifereji ya maji, sehemu za watembea kwa miguu na Taa za Barabarani.*
Pamoja na hayo *RC Makonda* amesema katika *uongozi wake hawezi kufumbia macho matumizi mabovu ya fedha za walipa kodi* hivyo atahakikisha anasimama *kidete* kuhakikisha *Dar es salaam inakuwa na barabara zenye ubora.*
Sanajari na hayo *RC Makonda* ametaka uwepo wa ushirikiano wa kikazi baina ya *TARURA, TANROAD, TANESCO, DAWASCO na TTCL* ilikupunguza *ucheleweshaji* wa miradi na ujenzi usiofuata taratibu unaopelekea *uharibifu wa miundombinu.
LENGO LA RC MAKONDA NI KUHAKIKISHA PESA YA WALIPA KODI INATUMIKA KUONDOA KERO WANANCHI
0 comments:
Post a Comment