Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege akikagua ujenzi wa kituo cha afya Mbwera.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege akikagua ujenzi wa kituo cha afya Mbwera.
Ujenzi wa kituo cha Afya Mbwera ukiendelea
...............................................................
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege ametoa miezi miwili kwa Kamati ya Usimamizi wa Ujenzi na Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya cha Mbwera kilichopo katika Halmashauri hiyo Mkoa wa Pwani.
Ametoa agizo hilo wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Mbwera kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi ambapo Serikali ilitoa shilingi milioni 400 na shirika la misaada la Korea shilingi milioni 149.
Mhe. Kandege amesema hajarizishwana kasi ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mbwera kwa kuwa mpaka sasa kipo katika hatua za msingi wa majengo mawili kati ya matano yanayotakiwa kujengwa huku gharama iliyotumika ni takribani shilingi milioni 120.
Amemuagiza Mhandisi wa ujenzi Bw. Jacob Mwakyambiki na mganga Mkuu wa Wilaya Bw. Martin Mwandiki kuhakikisha wanaweka kambi kwa ajili ya kusimamia Ujenzi huo ili ukamilike kwa wakati
Mhe. Kandege amewataka viongozi wa Kata na Vijiji kutimiza wajibu wao kwa kuisimamia ipasavyo Kamati ya ujenzi na kuwashirikisha wananchi katika kila hatua ya ujenzi wa majengo hayo ili thamani ya pesa inayotolewa na Serikali iweze kulingana na majengo yaliyojengwa.
Aidha ameuelekeza uongozi wa Mkoa wa Pwani kusimamia kwa karibu na kufuatili matumizi ya fedha zilizotumika hadi sasa ili kubaini iwapo kuna ubadhilifu wowote wa fedha na kuchukua hatua stahiki.
0 comments:
Post a Comment