Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza wakati akisoma taarifa ya Utekelezaji wa kazi zake kwenye Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Dodoma Mjini kwa mwaka 2015-2017.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa kazi zake kwenye Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Dodoma Mjini kwa mwaka 2015-2017.
Mbunge wa Viti maalum Felister Bura akizungumza katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Dodoma Mjini.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akipokea cheti maalum cha kutambua mchango wake alioutoa wakati wa uchaguzi wa viongozi wa CCM wilaya ya Dodoma mjini katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Dodoma Mjini.
wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Dodoma Mjini.
wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Dodoma Mjini.
wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Dodoma Mjini.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee mkoa wa Dodoma Balozi Job Lusinde akizungumza katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Dodoma Mjini.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Godwin Mkanwa akionesha mara baada ya kuzindua gazeti maalum la Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde linalojulikana kwa jina la Jimboni Kwangu ambalo linazungumzia habari mbalimbali za jimbo hilo.
......................................................................................
Mbunge wa Dodoma Mjini
Anthony Mavunde amesema hadi sasa ametekeleza zaidi ya asilimia 70 ya ahadi
zake alizozitoa wakati wa kampeni mwaka 2015 na kuwahakikishia wakazi wa Jimbo
lake hilo kuwa atahakikisha wanapata huduma zote muhimu kama alivyoahidi.
Akiwasilisha taarifa
ya Utekelezaji wa kazi zake kwenye Halmashauri Kuu ya Chama cha
Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Dodoma Mjini kwa mwaka 2015-2017.
Mavunde amesema kwa
kipindi cha miaka miwili tangu wananchi wa Jimbo hilo wamchague ameweza
kutekeleza ahadi mbalimbali alizozitoa.
Katika kikao hicho,
Mavunde ameeleza mafanikio makubwa na utekelezaji wa ahadi zake katika sekta ya
elimu, Afya, Maji, Miundombinu, Nishati na Uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Amewahakikishia
wananchi hao kuwa ataendelea kutatua kero mbalimbali zinazowakabili katika
sekta ya afya ili waweze kupata huduma bora.
Aidha amesema kuna
uboreshaji wa miundombinu ya maji unatarajiwa kufanyika katika vijiji
mbalimbali vya jimbo hilo na inakadiriwa kugharimu kiasi cha Sh.Milioni 800.
Ameeleza kuwa maombi
mengi yamepelekwa kwa wafadhili juu ya ufadhili wa miradi ya maji mijini na
vijijini.
Hata hivyo, amesema
katika uwezeshaji wananchi kiuchumi amekuwa akitoa mafunzo ya ujasiriamali na
kwasasa anatarajia kutoa kwa kila kata ili kuwapatia wananchi ujuzi.
Akizungumzia sekta ya
ardhi, Mavunde amesema katika ardhi ameendelea kushughulikia migogoro ya ardhi
ya mtu mmoja mmoja au kikundi kwa kutenga siku maalum ya kusikiliza kero za
wananchi kila Alhamis ya wiki.
Kufuatia taarifa hiyo,
Viongozi mbalimbali wa CCM wa Mkoa huo walimpongeza kwa hatua hiyo na kuwataka
wabunge wengine waige mfano huo.
Katika kikao hicho pia
alialikwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye amesema
Tanzania kuna wabunge wengi sana wanaotokana na CCM lakini Mavunde anatosha
sana.
“Ulipokuwa unasema
utekelezaji wa Ilani umefanya mambo makubwa sana uliyoyafanya wananchi wa
Dodoma wana kila sababu ya kushukuru, haya mazuri ambayo yameelezwa na mbunge
tusijifungie tukaeleze wananchi, uendelee kuwasaidia wananchi wako,”amesema
Aweso.
Amewahakikishia
wananchi kuwa watapata maji safi na salama na yenye kutosheleza.
0 comments:
Post a Comment