Mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula leo amezungumza na halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi ya kata ya Kirumba kufafanua juu ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kwa kipindi cha miaka miwili tangu kuchaguliwa kwake ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya utekelezaji wa Ilani kwa kata zote 19 za jimbo lake aliyoianza mwanzoni mwa mwaka huu 2018
Akiwa kata ya Kirumba amefafanua juu ya miradi mbalimbali iliyotekelezwa ndani ya kata hiyo ikiwemo utengaji wa fedha kwaajili ya vikundi vya vijana, wakinamama na walemavu, uibuaji wa vipaji kupitia michezo kwa kuanzisha Jimbo Cup, ufafanuzi juu ya matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo,utengwaji wa fedha kiasi cha milioni 700 kwaajili ya kituo cha afya Kirumba,ujenzi wa mradi mkubwa wa maji, ujenzi wa vyoo vya kisasa kwa shule ya msingi Kirumba, utekelezaji wa mradi wa huduma ya tiba kwa kadi, ukarabati wa barabara na kusisitiza juu ya zoezi la urasimishaji ambapo amewataka wananchi wake kuitumia vizuri fursa ya kurasimishiwa makazi yao kwa kulipia gharama za upimaji na hati miliki
'... Ndugu zangu zoezi la urasimishaji si zoezi endelevu lina muda, Muda ukipita zoezi hili halitakuwepo tena sasa ni aibu mbunge wenu ndie naibu waziri wa ardhi na Kirumba ndo nyumbani alaf ndo mnaongoza kwa kutorasimishiwa makazi yenu, ukiwekewa vigingi tu bila hati miliki haimaanishi ndo zoezi limekwisha hakikisheni mnalipia hati miliki ...' Alifafanua
Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula ameongeza kuwa zaidi ya watu 3106 wameshapimiwa ndani ya kata hiyo kukiwa hakuna aliyekwisha lipia gharama za umilikishwaji pamoja na kuwataka wakazi wa mtaa wa Kabuhoro kuwa wavumilivu wakati Serikali ikiendelea na utatuzi wa mgogoro wao wa ardhi wa muda mrefu nakuwasisitiza wasifanye maendelezo yoyote katika eneo hilo
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Mhe Alex Ngusa pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi kata ya Kirumba mbali na kumshukuru mbunge huyo wamemuahidi ushirikiano katika kuhakikisha utekelezaji wa Ilani unakwenda vizuri ndani ya kata yao na kuwataka wananchi na wanachama wa CCM kuendelea kumuunga mkono
Ziara hiyo ya utekelezaji wa Ilani pia ilihudhuriwa na mwenyekiti wa UVCCM Taifa Comred Kheri James, Viongozi wa CCM wilaya ya Ilemela na Jumuiya zake
' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
11.03.2018
0 comments:
Post a Comment