Vijana wametakiwa kuitumia michezo kama nyenzo katika kupambana na changamoto ya ajira
Kauli hiyo imetolewa leo na mgeni rasmi katika Bonanza la mchezo wa mpira wa miguu Comred Yusuph Ludimo lililoikutanisha Timu ya Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi wa kata ya Mkolani dhidi ya Timu ya Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi kutokea kata ya Mhandu lenye lengo la kuikaribisha sikukuu ya Pasaka na kudumisha Umoja, upendo na mshikamano kati yao ambapo amewaasa Vijana waliojitokeza katika mchezo huo kuona kuwa michezo inaweza kutumika kama nyenzo katika kupambana na changamoto ya ajira kwa Vijana wenyewe kujiajiri kupitia michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa miguu, Mpira wa Pete, michezo ya ngumi za kulipwa na mingineyo
'... Vijana wenzangu kama tutaamua kwa dhati ya moyo wetu kujikita katika michezo kwa nguvu zetu na maarifa yetu yote hatuwezi kulalamikia kuajiriwa, wenyewe mnafahamu kwasasa ajira zilivyokuwa changamoto lakini kama tutaamua kujikita katika michezo basi hii itakuwa njia mbadala katika kupambana na changamoto ya ajira ...' Alisema
Kwa upande wake mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi kata ya Mkolani Ndugu Kelvin Nyanza mbali na kumshukuru Comred Yusuph Ludimo kwa kukubali kuwa mgeni rasmi wa Bonanza hilo amewataka vijana wa kata ya Mhandu kuzidisha ushirikiano na vijana wa kata yake si tu katika michezo bali hata kushiriki pamoja katika kubuni miradi ya pamoja katika kujikwamua kiuchumi
Akihitimisha Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Mhandu Comred Musa Musa amewashukuru vijana wa kata ya Mkolani kwa kukubali kujumuika pamoja nao katika kufanikisha Bonanza hilo huku akiahidi ushirikiano na mshikamano kwa mambo mengine ya msingi yenye maslahi ya pamoja kwa vijana
Bonanza hilo la Mpira wa miguu lilianza kwa Timu ya Vijana CCM Kata ya Mkolani kuichapa Timu ya Vijana wa CCM Kata Mhandu goli 2-0, Huku goli la kwanza la Timu ya Mkolani likipatikana kupitia mchezaji wake Semeni Magige ambae pia ni mwenyekiti wa tawi la majengo baada ya kupokea Pasi kali kutoka kwa mjumbe wa mkutano mkuu wa mkoa kupitia kata hiyo Comred Mathias Mandiba kabla ya mchezaji Roby Chasam kutokea kata ya Mhandu kuipatia Timu yake goli la kusawazisha na mwishowe mchezaji nambari 9 Comred Amosy Boniface kuiongezea Timu yake ya Mkolani goli la pili na la ushindi
' Michezo ni afya, Michezo ni ajira '
0 comments:
Post a Comment