Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo akizungumza katika shughuli ya kupokea vifaa
vya shule kwa ajili ya watoto wenye ulemavu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo akipokea baadhi ya vifaa vya kuwasaidia
watoto wenye ulemavu kutoka kwa Mkurugenzi wa shirika la ADD Bi.Rose.
Viongozi mbalimbali wakiwemo watendaji wa ADD walioshiriki zoezi
la ugawaji vifaa vya watoto wenye ulemavu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo ameagiza mikoa yote kukamilisha uundwaji wa
kamati za walemavu kwa ngazi za mkoa, wilaya, na kata kabla ya mwisho wa mwaka
wa fedha 2017/2018.
Jafo ametoa agizo hilo alipokuwa akipokea vifaa vya kufundishia
watoto wenye ulemavu mbalimbali kutoka kwa Shirika la kimataifa linaloshughulikia
walemavu la ADD.
Amesema amelazimika kutoa agizo hilo kutokana na na kusuasua kwa
uundwaji wa kamati hizo ambazo zimeelekezwa kwa mujibu wa sheria.
Naye,Mwenyekiti wa Shirikisho la watu wenye ulemavu Tanzania,
Ummy pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la ADD Rose, wameipongeza Serikali ya awamu
ya tano chini ya Dk. John Magufuli kwa kuwajali sana walemavu hapa nchini.
Hata hivyo wameomba kuendelea kushughulikia changamoto
ambazo bado zinawakabili watoto zikiwemo uchakavu na upungufu wa miundombinu
hususan vyumba vya madarasa, vifaa vya kutosha vya kujifunzia, pamoja na mazingira
wezeshi kwa walemavu hususan baadhi ya miundombinu inayojengwa kutokuzingatia
mahitaji ya walemavu.
Katika zoezi hilo, Shirika la ADD limesaidia vifaa mbalimbali
vya kuwawezesha watoto wenye ulemavu kusoma vizuri vyenye thamani
ya sh. milioni 174.
0 comments:
Post a Comment