Judith Ferdinand, Mwanza
Wakulima mkoani Mwanza wamehimizwa kuchukua tahadhari ya wadudu ambao wanaharibu mazao mbalimbali mashambani walioingia nchini.
Dalili za kwanza za mazao kuliwa na wadudu hao ni majani ya mimea kuonekana yanamatundu matundu hivyo wanachi wachukue tahadhari wakiona dalili hizo kwa kupilizia dawa.
Tahadhari hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Kilimo na Uvuvi, Charles Tizeba katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoani Mwanza (RCC) Mwanza na kubainisha kwamba wadudu wa aina hiyo siyo sawa na wadudu wa kawaida ambao wamezoeleka ila zipo dawa aina tano kwa ajili ya kuulia wadudu hao.
Tizeba alisema,ametoa tahadhari kwa sababu wadudu hao watakula pamba, mahindi maharage na kila aina ya mazao.
Alisema, wadudu hao wametokea nchi za Kusini mwa Afrika na kuenea hapa kwetu, hivyo tusipo chukua hatua kwa pamoja watakula mazao yetu, kwani mwaka jana nchini Zambia walikula nusu ya mazao.
Pia alisema, kuna baadhi ya maeneo wameisha anza kushambulia mazao ikiwemo wilaya ya Biharamulo,Mleba na Mwanza kidogo,hivyo katika mikoa minne ambayo ametembelea amewaagiza Wakuu wa mikoa na wilaya zote, waweze kuweka amri halali ya wananchi kupulizia dawa kwenye mashambani kwao mara dalili za kuonekana wadudu hao wanashambulia mazao yao kwani akipulizia mmoja itakua ni kazi bure maana wadudu hao watahamia kwenye mashamba mengine.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela alisema, amepita baadhi ya wilaya mkoani hapa ikiwemo Magu, Misungwi na Ilemela na kuona baadhi ya mazao yameanza kushambuliwa na wadudu hao hasa mahindi.
Hivyo Mongela aliwaagiza Wakuu wa Wilaya kufikia januari 2 mwaka 2018, wahakikishe Watendaji wa Vijiji na Kata wanaelekezwa namna ya kupulizia dawa mashambani, kwani hawatakiwi kusubili tatizo mpaka litokee.
0 comments:
Post a Comment