METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, January 3, 2018

DKT ANGELINE MABULA ATEMBELEA MIRADI YA UHIFADHI MAZINGIRA (LVEMP)

Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula ametembelea mradi wa Ujenzi wa Vyoo kwa Shule ya Msingi Buzuruga, Shule ya Msingi Nyambiti na Shule ya Msingi Isenga iliyojengwa  kwa ufadhili wa Serikali kuu (Wizara ya Maji) ikishirikiana na Benki ya Dunia kupitia mradi wa Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira ya Ziwa Viktoria ( LVEMP )

Akizungumza mara baada ya kutembelea mradi huo Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kushukuru kwa Ujenzi wa miradi  ndani ya Jimbo lake amewataka wananchi kutoa ushirikiano na kuitunza ili iwanufaishe kwa muda mrefu huku akiomba kusaidiwa ujenzi wa Vyoo vipya na vya kisasa katika maeneo ya Mialo ya Ziwa Viktoria inayopatikana Ilemela sambamba na sehemu za kisasa za kukaushia Samaki pindi wanapovuliwa

‘… Tunawashukuru wenzetu wa LVEMP kwa mradi huu lakini pia tumewaomba na watatusaidia, Lengo langu kubwa ni kule kwenye maeneo ya mialo unajua kule nako kuna uhitaji mkubwa wa kuwa na vyoo, Lakini kuna uhitaji mkubwa zaidi wa kuwa na maeneo ya kuwa wanaweza kukaushia samaki wao vizuri katika vichanja vya kisasa ambavyo ni rafiki wa mazingira …’ Alisema

Kwa upande wake mratibu mradi huo waUtunzaji mazingira ya Ziwa Viktoria  LVEMP Ndugu  Omary Mnyanza amefafanua juu ya lengo kuu la mradi ambalo ni uhifadhi na utunzaji wa mazingira na kusaidia afya za wananchi huku akimhakikishia Mhe mbunge wa Jimbo la Ilemela  juu ya utekelezaji wa ombi lake la ujenzi wa Vyoo vya Kisasa na Vichanja vya kukaushia Samaki maeneo ya Mialo ya Ilemela na kuhitimisha kwa kuwataka wananchi kuacha kujisaidia ovyo na kuchafua Ziwa Viktoria

‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
02.01.2017

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com